Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watano wafariki, 54 wajeruhiwa ajali ya basi Shinyanga
Habari MchanganyikoTangulizi

Watano wafariki, 54 wajeruhiwa ajali ya basi Shinyanga

Spread the love

 

WATU watano wamepoteza maisha huku 54 wakijeruhiwa Katika ajali ya Basi lililogongana na Fuso  uso kwa uso eneo la Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea).

Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi Septemba 3,2022 majira ya saa 8 usiku, ikihusisha basi  kampuni ya Super Najimunisa yenye namba za usajili T.413 DAY likitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza, na Fuso yenye namba za usajili T.123 DJH lililokuwa ikitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam likiwa na mzigo wa dagaa.

Manusura wa ajali hiyo Fred Mahina, amesema dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha mwendokasi na walipokuwa wakimzuia aliwajibu wangetaka usafiri wa raha wangepanda ndege, huku akiwaambia wasali sana ili wafike salama.

“Tulipofika Morogoro dereva akiwa mwendokasi alikwaruza Roli tukapona kuanguka, lakini akazidi kuendesha mwendokasi abiria tulipokuwa tukipiga kelele apunguze mwendo, aligoma na kutuambia tusali ,ndipo tulipofika hapa Shinyanga na kupata ajali,” anasema Mahina.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Leonard Nyandahu ambaye alikuwa eneo la ajali hiyo, amesema chanzo ni uzembe wa dereva wa basi kwa kutozingatia vibao vya usalama barabarani na kuendesha mwendokasi.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga, Dk. Luzila John amethibitisha kupokea miwili ya watu watano pamoja na majeruhi 54 ambao wanaendelea na matibabu.

Amesema miili ya hao marehemu hao bado haijatambuliwa majina yao, na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!