Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ubalozi wa Marekani nchini Kenya watoa tahadhari kwa raia wake
Kimataifa

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya watoa tahadhari kwa raia wake

Spread the love

 

UBALOZI wa Marekani nchini Kenya umewataka raia wake kuchukua tahadhari kubwa nchini humo wakati huu ambapo , mahakama ya juu inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uchaguzi wa Urais mnamo tarehe 5 Septemba 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Ubalozi huo umesema kwamba Kenya imekuwa ikikumbwa na msusuru wa ghasia kila baada ya uchaguzi.

Taarifa hiyo hususan imewataka maafisa wake waliopo katika mji wa Kisumu kuchukua tahadhari wakati ambapo uamuzi huo utakuwa ukifanywa na mahakama ya juu.

‘’Uchaguzi unaohusishwa na maandamano na mikutano mara kwa mara hutokea baada ya uchaguzi, na mara nyengine husababisha trafiki barabarani kutokana na maandamano ambayo hushirikisha ghasia hali ambayo uhitaji maafisa wa polisi kuingilia kati’’, ilisema Taarifa hiyo.

Kisumu ni mji wa eneo anakotoka mmoja wa wagombea urais Raila Odinga ambaye ameiomba mahakama kubatilisha tangazo la William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!