Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Raila Odinga afungua rasmi kesi ya kupinga uchaguzi wa urais
Kimataifa

Raila Odinga afungua rasmi kesi ya kupinga uchaguzi wa urais

Raila Odinga
Spread the love

 

MGOMBEA wa urais nchini Kenya, kupitia Muungano wa Azimio, Raila Odinga, hatimaye amewasilisha rasmi ombi la kupinga uchaguzi wa William Ruto kuwa rais mteule. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kenya … (endelea).

Kesi hiyo iliwasilishwa na mawakili wa Raila walioongozwa na wakili James Orengo katika mahakama ya upeo ya Milimani.

Sheria kuhusu kesi ya kupinga uchaguzi wa Urais 2017 inasema, iwapo kesi itawasilishwa katika siku ya mwisho ya muda uliowekwa kuwasilisha kesi hiyo, basi ni sharti ifanyike kabla ya saa nane mchana ya muda uliowekwa.

Kulingana na wakili wa Muungano wa Azimio Daniel Maanzo, kikosi cha mawakili tayari kimewasilisha kesi hiyo mtandaoni na kwamba watawasilisha stakhabadhi zinazohitajika mahakamani wakati wowote kufikia sasa.

Alisema: “Tumewasilisha kesi hiyo kupitia mtandao huku tukisubiri kuleta stakhabadhi ili mahakama hiyo iweze kuthibitisha ombi hilo.”

Aliongeza: “Tuna hadi saa nane, lakini naweza kuwahakikishia kwamba kila mtu yuko tayari. Kundi la mawakili linaendelea kukusanya nakala za kesi hiyo na zinatarajiwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.”

Kufuatia hatua ya kuwasilisha kesi hiyo mahakamani, Muungano wa Azimio una hadi tarehe 23 Agosti, kukikabidhi chama cha UDA, rais Mteule na tume ya uchaguzi IEBC malalamishi hayo.

Na hayo yakijiri wafuasi wa Muungano wa Azimio wamekongamana nje ya mahakama hiyo ya milimani ili kuunga mkono azma ya viongozi wao, kuwasilisha kesi hiyo.

Usalama meimarishwa nje ya mahakama hiyo.

13 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!