Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Salman Rushdie apumulia mashine baada ya kuchomwa visu Marekani
KimataifaTangulizi

Salman Rushdie apumulia mashine baada ya kuchomwa visu Marekani

Spread the love

MWANDISHI wa habari mzaliwa wa Mumbai nchini India, Salman Rushdie, anapumulia mashine hospitalini baada ya jana tarehe 12 Agosti, 2022 kushambuliwa na visu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Shambulio hilo lilitokea wakati akijitayarisha kutoa mhadhara jijini New York.

Mashahidi wanasema, mshambuliaji alipanda kwenye jukwaa ghafla na kumchoma visu mara kadhaa mwandishi huyo wa kitabu cha Aya za Shetani.

Wakala wake, Andrew Wylie, anasema Rushdie amejeruhiwa ini, mishipa ya damu na huenda akapoteza jicho moja.

Polisi inamshikilia mshambuliaji iliyemtaja kwa jina la Hadi Matar, mwenye umri wa miaka 24.

Rushdie, mwenye umri wa miaka 75, ameishi miaka mingi akiwa chini ya ulinzi wa polisi, kutokana na fatwa ya kifo dhidi yake iliyotolewa mwaka 1989 na kiongozi mkuu wa wakati huo wa Iran, Ayatullah Khomeini, baada ya mwandishi huyo kuandika riwaya yake ya nne, Aya za Shetani, ambayo inatajwa kuukashifu Uislamu.

Ingawa baadaye Iran ilijitenga na fatwa hiyo, lakini mwaka 2015, Wakfu wa 15 Khordad wa nchi hiyo ulitangaza zawadi ya dola milioni 3.3 kwa yeyote atakayemuuwa Rushdie.

Haijaweza kufahamika mara moja, mtekelezaji wa shambulio hilo alikuwa na malengo gani.     Salman Rushdie, mwandishi wa fasihi ambaye amekuwa akikabiliwa na kitisho cha kuuawa kutokana na uandishi wake; amekuwa akiishi kwa kutisho kwa karibu miongo mitatu sasa.

Mwandishi huyo wa fasihi alipangiwa kuzungumzia uhuru wa wasanii mbele ya hadhara ya mamia ya watu, alipovamiwa na mtu aliyefunika uso kwa barakowa.

Maafisa wa polisi waliokuwa katika ukumbi wa mkutano huo, waliingilia kati na kumtia mbaroni mshambuliaji.

Gavana wa New York, Kathy Hochul amelilaani shambulizi hilo, na amearifu kuwa Rushdie yuko hai na anaendelea kupatiwa matibabu.

Ama kuhusu hali ya afya yake, imearifiwa kuwa anapumua kwa kutumia mashine, na amepata majeraha mabaya usoni, shingoni na tumboni.

Polisi lakini wamesema bado hawajajua malengo ya mshambuliaji wake, wala kubainisha aina ya silaha aliyoitumia.

Hata msemaji wake amesema kupitia taarifa ya baruapepe kuwa mwandishi huyo anafanyiwa upasuaji bila kutoa maelezo zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Spread the loveMBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

error: Content is protected !!