Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yairarua Simba, Mayele atetema
MichezoTangulizi

Yanga yairarua Simba, Mayele atetema

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya YANGA imeanza vema msimu mpya kwa kutetea taji lao la Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mtani wake Simba. Anaripoti Urumasalu Kisung’uda, TUDARCo … (endelea).

Mabao ya Yanga katika mchezo huo uliopigwa leo tarehe 13 Agosti, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na mshambulia hatari, Fiston Mayele ambaye amemtungua Beno Kakolanya dakikika ya 50 na 80.

Aidha, bao pekee la Simba lilifungwa na Pape Sakho dakika ya 16.

Simba walianza kipindi cha kwanza kwa kutawala mchezo huo kwa kupiga mashuti manne yaliyolenga lango la Yanga ilihali Yanga wakiwa na shuti moja pekee.

Wakati dakika 45 zilikatika Simba walienda mapumziko wakiwa wanajiamini hasa baada ya kutawala ungwe hiyo ya kwanza.

Mabadiliko ya Bernard Morrison ambaye aliingia kipindi cha pili na Jesus Moloko yaliongeza nguvu upande wa kiungo.

Zoran Maki alizidiwa mbinu na uzoefu na Nasreddine Nabi ambaye ameweza kuwaongoza vijana wake kupindua meza kibabe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!