Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TPA yatangaza vipaumbele muhimu 5
Habari Mchanganyiko

TPA yatangaza vipaumbele muhimu 5

Spread the love

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari TPA imesema ujenzi wa miundombinu bora ya Bandari yenye mitambo ya kisasa  na sahihi ya kuhudumia meli na shehena ni mojawapo ya vipaumbele vitano ambavyo viko kwenye Mpango Mkakati wake wa Nne wa mwaka 2021/22-2025/26) wa mamlaka hiyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 13 Agosti, 2022 na Mkurugenzi wa Mipango, ubora na Uthibiti vihatarishi Dk. Boniface Nobeji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mipango ya utekelezaji wa bajeti katika mwaka wa fedha 2022/23.

Aidha, amesema katika vipaumbele hivyo wanakusudia kuongeza shehena ya  nchi jirani  inayohudumiwa na bandari  za Tanzania na kuimarisha masuala ya ulinzi, usalama na mazingira katika utoaji wa huduma pamoja na kuzingatia miongozo ya kimataifa iliyoridhiwa na nchi.

Ameeleza kuwa vipaumbele hivyo vinatekelezwa na TPA kupitia Mipango na bajeti za kila mwaka.

Kuhusu shehena ya magari iliyohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022 ilikuwa 203,932 sawa na ongezeko la asilimia 38 ya magari 147,566 yaliyohudumiwa mwaka uliopita (Julai 2020 hadi Juni  2021).

Dk. Nobeji ameeleza kuwa ili kuendelea kutekeleza vipaumbele ilivyojiwekea, katika mwaka wa Fedha 2022/2023, TPA imetenga bajeti yake kwa malengo mbalimbali.

Ameyatenga malengo hayo kuwa  lengo la kwanza ni ukusanyaji wa mapato  Jumla ya sh.bilioni 1,224.405.

Pia matumizi ni sh.bilioni  866.051 na ziada ya sh.bilioni  358.354 kabla ya kodi.

Aidha, ameeleza kuwa bajeti ya miradi ya uwekezaji ikiwemo vitendea kazi ni sh.bilioni 762.606 na sh.bilioni 662.493  ni mapato ya ndani huku sh. bilion 100.112 ikitoka Serikalini (Ruzuku kwa utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!