Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia: Tone moja la maji ni Sh 3,000
Habari za Siasa

Samia: Tone moja la maji ni Sh 3,000

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema maji yangeuzwa kwa kuangalia gharama za miradi tone moja la maji lingeuzwa kwa Sh 3,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Badala yake Mkuu huyo wa nchi amesema Serikali inawekeza fedha nyinge kwenye miradi ya maji ili wananchi wafaidike na huduma hiyo.

Ameyasema hayo leo Ijumaa ttarehe 5 Agosti, 2022, wakati akizungumza na wananchi wa Mbalizi mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Shongo-Mbalizi uliogharimu Sh 3.3 bilioni.

Amesema kutokana na gharama kubwa za miradi ndiyo sababu ya sekta binafsi kutowekeza katika miradi ya maji na badala yake Serikali ndiyo inatoa huduma hiyo.

Akifafanua zaidi amesema hivi sasa wannchi watannua uniti mopja yam aji ambayo ni sawa na ndoo 50 za lita 20 kwa Sh 1,100 tofauti na awali ambapo walikuwa wakiuziwa ndoo moja kwa Sh 500.

“Kutokana na gharama za miradi ya maji tone moja la maji lingeuzwa kwa Sh 3,000, tone moja sio hata lita moja. Lakini hapa ndoo 50 za lita 20 tunauziwa Sh 1100, wakati mkinunua maji mlikua mnanunua dumu moja Sh 500…sasa hiyo ndo kazi ya Serikali kuweka fedha wananchi wake wafaidike ndo maana sekta binafsi haipo kwenye maji,” amesema Samia.

Mradi wa maji wa Shongo-Mbalizi uliopo mkoani Mbeya umegharimu Sh3.345 bilioni na utazalisha lita milioni 8-12 za maji kwa siku ukihudumia wakazi 80,000 wa eneo la Mbalizi.

Mradi huo wenye mtandao wa mabomba wa kilomita 49 umeongeza upatikanaji wa maji katika eneo la Mabalizi kutoka asilimia 44 hadi 95 ambapo wateja 9,985 wameunganishwa na huduma ya maji kutoka wateja 5,436 wa awali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!