August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nandy aanika vituko vinavyotokana na ujauzito wake

Spread the love

 

MSANII maarufu nchini Tanzania Nandy ameelezea kwa uwazi vituko anavyofanya kutokana na hali yake ya ujauzito. Anaripoti Juliana Assenga, UDSM … (endelea).

Nandy amefunguka na kusema toka apate ujauzito amekuwa hawapendi marafiki wa mume wake, na kupelekea kutoelewana nao, pia anasema nyakati zingine amekuwa hata akipokea simu zake na kuongea nao.

Msanii huyu pia anadai kuwa amekuwa akikwazika na kulia sana kiasi cha hata kumpelekea kutokula kwa siku mbili. Anasema amekuwa hivo hasa pale anaposemwa kidogo na mtu anaposhindwa kujirudi na kumuomba msamaha.

Nandy ambaye alikuwa akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Wasafi amesema toka awe mjamzito amekuwa akipendelea kula chips maarufu kama Chips za Dubai mida ya saa 9 usiku.

Anasema kuwa hupendelea kula chips hizo kila ahisipo njaa na kuwa anaweza kuzila mara nyingi kwa siku hata akiwa amekwisha kula chakula cha jioni.

error: Content is protected !!