Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia kuhusu bei ya mafuta: Ni tatizo la dunia nzima
Habari za Siasa

Samia kuhusu bei ya mafuta: Ni tatizo la dunia nzima

Spread the love

 

WANANCHI wa Mbalizi mkoa wa Mbeya nchini Tanzania amemuhoji Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta ambapo amewajibu kuwa licha ya jitihada za Serikali kuweka ruzuku, bei ya mafuta imekuwa ni tatizo la dunia nzima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Rais huyo ameyasema hayo leo Ijumaa tarehe 5 Agosti akizungumza na wananchi wa eneo hilo ambapo amesema tatizo hilo litaendelea hadi dunia itakapoacha kupigana na bei za mafuta kushuka katika soko la dunia.

Vinginevyo amesema Serikali italazimika kukata fedha za miradi ya maendeleo na kuzipeleka kuweka ruzuku ili bei ya mafuta isiendelee kupanda.

“Mafuta ya magari yanaendelea kupanda bei duniani, hatua tuliyochukua kama Serikali ni kutafuta ruzuku ya kushusha bei ya mafuta, tungeachia mafuta yapande bei kama yanavyokwenda duniani mafuta yasingenunulika,” amesema Samia.

Amesema Serikali inatoa Sh 100 bilioni kila mwezi kama ruzuku kwenye mafuta ili bei zisiendelee kupanda, “mpaka huko duniani waache kupigana, mpaka huko duniani bei zianze kushuka ndiyo tutapata unafuu.”

Amesema bei ya mafuta inaendelea kupanda duniani, “lakini sisi tunashusha kwa kutoa ruzuku na Serikali ipo macho tunafanya kuhakikisha bei isipande kiasi kile kilichopanda kwa wenzetu.”

Amesema kwenye nchi zingine za Afrika Mashariki mafuta “hayanunuliki, lakini marais wote tunajitahidi kwa njia yeyote kila mmojakwa namna yake kupunguza bei ya mafuta, bei ya mafuta ni tatizo la ulimwengu mzima tunajitahidi bei zibakie pale zilipo kwa hiyo kuhusu mafuta Serikali yenu tunahangaika.”

Bei ya mafuta imepanda tena mwezi huu na kuivuka ile ya Julai 2022, ambapo petroli imepanda kwa Sh190 kwa kila lita na Sh 179 kwa kila lita ya dizeli huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh 323 kwa kila lita katika jiji la Dar es Salaam.

Kwa mkoa wa Mbeya bei ya petroli ni Sh 3,533, dizeli Sh 3,445 na mafuta ya taa Sh 3,888 ikiwa ni bei baada ya ruzuku.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!