Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wa dini watakiwa kuliombea Taifa
Habari Mchanganyiko

Viongozi wa dini watakiwa kuliombea Taifa

Spread the love

VIONGOZI wa dini wametakiwa kusimama imara na kuliombea Taifa pamoja na viongozi wakuu wa ili wasikengeuke na kuruhusu shetani kuwashambulia na kuacha mapenzi ya Mungu.

Wito huo umetolewa na leo tarehe 31 Julai, 2022 na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches (TFC), Dk. Godfrey Malassy wakati akiongoza ibada maalumu ya maombi ya kuliombea Taifa pamoja na viongozi wa ngazi ya juu ya kitaifa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)

Mbali na mambo hayo pia kanisa hilo limetoa vyeti na tuzo kwa wadau ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuwezesha maandalizi ya mikesha ya kuliombea yaifa na kuwaombea viongozi wakuu wa nchi.

Kiongozi hiyo wa kiroho ameeleza kuwa ili nchi iongozwe vizuri ni lazima iwe na viongozi ambao ni wacha-Mungu na wenye hofu ya Mungu ambao wanajali maisha ya watu wanaowaongoza badala ya kuangalia matumbo yao.

Aidha ameeleza kuwa taifa linatakiwa kutambua kuwa uchumi uliopo ni uchumi wa watanzania wote kwa faida kubwa na siyo kwa faida ya watu wachache.

Katika hatua nyingine kanisani limetoa tuzo na vyeti kwa wadau mbalimbali waliokuwa mstari wa mbele katika kuwezesha ufanikishaji wa mikesha ya dua na maombezi kwa taifa ambayo ufanyika kila mkesha wa kuhamkia mwaka mpya.

“Tunatambua mchango mkubwa wa wadau ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha mikesha ya maombi kwa kutoa muda wao,mali pamoja na mawazo yao.

“Tunatambua umuhimu wenu na tutaendelea kushirikiana vyema kwani nia yetu ni kuona nchi imakuwa na utulivu na kila mmoja anakuwa na amani na upendo kwa mwenzake, nchi isiyokuwa na wala rushwa au matendo ya kikatili,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!