August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Djuma Shaban asalia Yanga kwa mwaka mmoja Zaidi

Spread the love

 

Mabjngwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya soka ya Yanga, imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja beki wake wa kulia Raia wa Kidemokrasia ya Congo, Djuma Shabani ambao unamfanya aendelee kusalia ndani ya kikosi hiko hadi 2024. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezaji huyo ameongeza mkataba wake hivi karibuni mara baada ya kurejea ndani ya kikosi hiko akitoka mapumzikoni.

Mkaba wa awali wa mchezaji huyo ulikuwa unamalizika kwenye msimu ujoa ambao unatarajia kuanza hivi karibuni, kufuatia kusaini miaka miwili hapo awali.

Tokalipofika nchini 2021, akitokea kwenye klabu ya AS Vita, Djuma amekuwa na msimu mzuri akiwa Yanga na alifanikiwa kuibuka kuwa kinara wa utoaji wa pasi za mwisho (assist).

Pia mchezaji alifanikiwa kuingia kwenye kikosi bora cha msimu, katika tuzo zilizotolewa na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) tarehe 7 julai 2022.

error: Content is protected !!