Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yatoa mamilioni maonyesho ya Nanenane, Dk Mpango kuyafungua
Habari Mchanganyiko

NMB yatoa mamilioni maonyesho ya Nanenane, Dk Mpango kuyafungua

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk. Rashid Mohamed Chuachua akipokea hundi ya Shilingi Milioni 60 kutoka Meneja wa Benki ya NMB Kanda Nyanda za Juu Straton Chilongola
Spread the love

 

WAKATI Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango akifungua maonyesho ya sikukuu ya wakumilima ‘nanenane,’ Benki ya NMB imetoa Sh.60 milioni kuchangia maonyesho hayo Kitaifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea). 

Dk Mpango anafungua maonyesho ya nanenane Kitaifa leo Jumatatu, Agosti 1,2022 jiji Mbeya na yakitarajiwa kufungwa na Rais Samia Suluhu Hassan Agosti 8, 2022.

NMB imekabidhi udhamini huo jana Jumapili na kufanya benki hiyo kufikisha kiasi cha Sh. 195 milioni ambazo imetoa kwa kipindi cha miaka mitano katika kufanikisha shughuli za manyesho hayo kitaifa.

Katika hafla ya kukabidhi hundi ya fedha hizo iliyofanyika mjini Mbeya, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini l, Straton Chilongola alisema benki hiyo imetoa kiasi cha fedha kwa ajili ya kufanikisha shughuli mbalimbali za maonyesho hayo.

“Kwetu kusaidia sekta ya kilimo ni fahari yetu kwani kupitia kilimo, benki hii imekuwa ikifanya biashara kubwa ambayo pia imechangia sana ukuaji wa sekta ya kilimo nchini na Mbeya kwa ujumla,” alisema Chilongola.

Alisema kwa miaka mitano ambayo maonyesho ya Nane Nane yamefanyika nchini, NMB imetoa udhamini wa zaidi ya Sh. 195  milioni fedha ambazo benki hiyo inaamini zinachangia pakubwa katika kufanikisha maonyesho hayo muhimu kwa taifa.

Aidha, Chilongola alisema  katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan, mchango wa NMB kama benki wakujenga uchumi imara kupitia kilimo na ufugaji ni ndani ya miaka minne, wamefungua zaidi ya akaunti 644,034 za wakulima nchi nzima.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ambaye alipokea hundi ya fedha hizo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera aliishukuru Benki ya NMB kwa kutoa kiasi hicho cha fedha ambacho alieleza kitawezesha maonyesho kufanyika kwa ubora.

“Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, nawashukuru sana viongozi wa Benki ya NMB kwa udhamini wao, tunaamini utatusaidia kuboresha maonyesho yetu,” alisema Dk. Chuachua.

Alisema tayari maonesho hayo yameanza na hivyo kuwataka wananchi wakiwemo wajasiriamali kutembelea mabanda na kwamba zipo kamati zinazoratibu taratibu mbalimbali kwenye maonyesho hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!