Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Mkenda awaaga Rais Museveni, Ndayishimiye
Habari Mchanganyiko

Prof. Mkenda awaaga Rais Museveni, Ndayishimiye

Spread the love

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni pamoja na Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye leo tarehe 23 Julai, 2022 kwa nyakati tofauti wameondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kuagwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Viongozi hao waliwasili nchini tarehe 21 Julai 2022 na kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kuanzia tarehe 21-22 Julai 2022 katika Ukumbi wa kimataifa wa mikutano-AICC Jijini Arusha.

Kadhalika, Viongozi hao waliungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),  Uhuru Kenyatta, katika ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!