Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Ummy: Ugonjwa wa homa ya mgunda unatibika
Habari MchanganyikoTangulizi

Waziri Ummy: Ugonjwa wa homa ya mgunda unatibika

Spread the love

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema ugonjwa wa homa ya Mgunda uliogundulika huko Ruagwa mkoani Lindi unaweza kuzuilika na unatibika. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ummy ameeleza hayo leo Jumatatu tarehe 18, Julai, 2022, akitoa taarifa ya ugonjwa huo ambao ulikuwa haujafahamika kwa muda wa siku 10 tangu kuripotiwa kwa watu wenye dalili za kuvuja damu puani na homa.

Waziri huyo amesema hadi jana tarahe 17, Julai, jumla ya visa 20 vilikuwa vimebainika huku idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo ikibakia watatu.

“Kwa sasa, wagonjwa wawili pekee wenye dalili ndiyo bado wamelazwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya matibabu,” amesema Ummy.

Amesema ugonjwa huo unaambukizwa na bakteria Leptospira interrogans kutoka kwa Wanyama wakiwemo panya, swala, kindi, mbweha, kulungu na wanyamapori wengine, kwenda kwa binadamu kupitia kugusana na majimaji kutoka kwa wanyama hao.

Umbo la bakteria Leptospira

Hata hivyo amesema maambukizi wa ugonjwa huo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ni ya nadra.

Ameongeza kuwa kwa Tanzania, ugonjwa huu si mpya, na ulishawahi kutokea mwaka 2014 katika Halmashauri ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Amesema mgonjwa aliyeambukizwa vimelea vya ugonjwa huo huanza kuonesha dalili katika kipindi cha kati ya siku tano hadi 14 na wakati mwingine dalili huweza kutokea kati ya siku mbili hadi 30.

“Wizara inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huu na kuendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu. Hivyo Serikali inawaasa Wananchi kutokuwa na hofu kwani ugonjwa huu unaendelea kudhibitiwa,” amesema Ummy katika taarifa hiyo.

Itakumbukwa kuwa tarehe 07 Julai 2022, Wizara ya Afya ilipokea taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi ya uwepo wa wagonjwa wenye dalili za homa inayoambatana na kutoka damu katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Kufuatia taarifa hizo, Wizara ilituma timu ya wataalam kutoka ngazi ya Wizara na wengine kutoka Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na taasisi zingine za afya.

Taarifa ya awali ya sampuli zilizopimwa katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii zilionesha majibu hasi kwa ugonjwa wa Ebola, Marburg na UVIKO-19. Vile vile, uchunguzi zaidi ulioendelea kwenye Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na Wakala wa Maabara ya Mifugo umeonesha majibu hasi kwa ugonjwa wa Influenza, Kimeta (Anthrax), Crimean Congo Hemorrhagic Fever (CCHF), Yellow Fever, Chikungunya, West Nile Virus na Rift Valley Fever.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!