Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Dk. Mpango aonya madaktari, watoa huduma afya kuzingatia maadili
Afya

Dk. Mpango aonya madaktari, watoa huduma afya kuzingatia maadili

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amewataka madaktari na watoa huduma wote nchini kuendelea kuwa wenye upendo, kujituma, kujitoa na kuzingatia weledi na maadili ya tasnia ya utabibu.

Dk. Mpango ametoa kauli hiyo jana tarehe 17 Julai, 2022 imetolewa wilayani Siha wakati akizungumza na watoa huduma wa afya pamoja na wananchi wa Wilaya hiyo.

Dkt. Mpango alisema kuwa anafahamu wako madaktari na wahudumu wa afya wengi wanaofanya kazi nzuri na wengine hata katika mazingira magumu na hatarishi.

“Mnafanya kazi ya Mungu na endeleeni kufanya hivyo bila kukata tamaa. Pamoja na Serikali kuendelea kuboresha maslahi yenu, nawasihi pia motisha yenu iwe katika kuona thamani ya maisha ya watu wengi mliyookoa kwa huduma za afya mnazotoa”.

Aidha, aliwataka madaktari na wahudumu wote kutumia utaalamu wao kutoa elimu ya afya na kinga.

Alisema ni wazi kuwa, gharama za tiba kwa mtu aliyepata maambukizi ya ugonjwa ni kubwa na wakati mwingine hazibebeki kwa watanzania walio wengi hivyo Wizara ya Afya, madaktari na wahudumu wa afya waongeze jitihada za kutoa elimu ya afya hususan ile inayolenga katika kuwakinga watanzania na magonjwa ya kuambukiza na hata yasiyoambukiza ili kuepuka gharama kubwa za matibabu.

“Kuweni wabunifu katika kutoa elimu, tumieni njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, teknolojia ya Habari na mawasiliano pamoja na mifumo ya kidigitali”Tukumbuke ule msemo wa wahenga wetu kuwa, “Kinga ni bora kuliko tiba”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!