Wednesday , 15 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri mkuu Sri Lanka ateuliwa kuwa Rais wa mpito
Kimataifa

Waziri mkuu Sri Lanka ateuliwa kuwa Rais wa mpito

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe ameteuliwa kuwa Rais wa muda baada ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Gotabaya Rajapaksa kukimbilia nchi jirani ya Maldives. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea)

Taarifa iliyotolewa na  Spika wa taifa hilo lililopo kusini mwa Asia, imesema Rais Rajapaksa alimfahamisha kuhusu uteuzi huo chini ya Kifungu cha 37.1 cha katiba ya Sri Lanka.

Hata hivyo, hakuna kauli ya moja kwa moja kutoka kwa Rajapaksa mwenyewe.

Kwa mujibu wa Katiba ya Sri Lanka, nafasi ya rais ikiwa wazi, waziri mkuu ataapishwa na kukaimu kwa muda mpaka atakapochaguliwa rais kutoka miongoni mwa wabunge.

Uchaguzi huo unapaswa kufanyika ndani ya siku 30 baada ya Rais kujiuzulu. Spika wa bunge la Sri Lanka alisema uchaguzi unaweza kufanyika tarehe 20 Julai, 2022.

Wakati leo ikiwa ndiyo siku aliyopaswa kutangaza kujiuzulu, imeelezwa kuwa Rais Rajapaksa (73) ameikimbia nchi hiyo kwa ndege ya kijeshi, huku kukiwa na maandamano makubwa yaliyotokana na mzozo wa kiuchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!