Polisi Uganda imewakamata waandamanaji 12 waliokuwa wakipinga kupanda kwa gharama ya maisha katika eneo la Jinja, lililopo kusini-mashariki mwa nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya kimataifa… (endelea)
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Polisi nchini humo jana tarehe 12 Julai, 2022, James Mumbi imesema viongozi wanane kati ya hao 12 pia walikamatwa na watafunguliwa mashtaka ya kuchochea ghasia nchini humo.
Waandamanaji hao, wanadaiwa kuchoma matairi na kufunga barabara yenye shughuli nyingi mjini Jinja na kuwalazimu madereva wa magari kuungana nao kutaka serikali iwape ruzuku ya chakula cha msingi.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi karibuni, kiwango cha mfumuko wa bei kwa bidhaa za chakula kimefikia asilimia 13.1 kwa mwezi Mei 2022.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, amewataka raia wake kuishi kwa mpangilio badala ya kupunguza ushuru na kuongeza misaada ya serikali kwa watu walio hatarini zaidi, kama wengi wanavyotaka.
Juni 2022, mwanasiasa wa upinzani na aliyekuwa mgombea urais, Kizza Besigye alifungwa jela na kushtakiwa kwa kuchochea ghasia kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja, baada ya kuongoza maandamano kadhaa kupinga kupanda kwa gharama ya maisha.
Leave a comment