Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mapato yaongezeka kwa 22.77%, TRA yataja sababu tano
Habari Mchanganyiko

Mapato yaongezeka kwa 22.77%, TRA yataja sababu tano

Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa TRA
Spread the love

 

MAKUSANYO ya mapato ya Tanzania, kwa mwaka wa fedha ulioisha wa 2021/22, yameongezeka kwa kwa asilimia 22.77, kutoka Sh. 18.15 trilioni (2020/21) hadi kufikia Sh. 22.28 trilioni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya ongezeko hilo imetolewa jana Julai Mosi, 2022 na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata, na kusambazwa leo Jumamosi tarehe 2 Julai 2022.

“TRA inapenda kuutarifu umma kuwa katika kipindi cha 2021/22, (Julai 2021 hadi Juni 2022), imefanikiwa kukusanbya kiasi cha Sh. 22.28 trilioni, ikiwa nin sawa na ufanisi wa asilimia 99.22 ya lengo la makusanyo ya Sh. 22.45. Makusanyo haya ni ongezeko la Sh. 4.13 trilioni, ikilinganishwa na kiwango cha makusanyo cha Sh. 18.15 trilioni, kilichofanyika kipindi kama hicho kwa 2020/21. Ongezeko hili ni sawa na ukuaji wa makusanyo kwa 22.77%,” imesema taarifa ya Kidata.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kidata, Juni 2022, TRA imekusanya Sh. 2.32 trilioni, kati ya lengo la kukusanya Sh. 2.05 trilioni,ikiwa ni ufanisi wa asilimia 113.17.

“Makusanyo haya ya mwezi Juni ni ukuaji wa asilimia 24.81, ikilinganishwa na makusanyo ya mwezi Juni 2021,” imesema taarifa ya Kidata.

Kidata ametaja sababu tano, zilizopelekea ongezeko hilo.

“Ufanisi huu wa kiutendaji ni matokeo ya kuendelea kuimarika kwa matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika usimamizi na ukusanyaji wa kodi, amzingira ya ufanyaji biashara nchini na mwenendo wa ulipaji kodi kwa hiari, uboreshwjai wa mahusiano baina ya TRA na walipakodi, utatuzi wa migogoro ya kodi nje ya mahakama na kuongezeka kwa kiwango cha uhamasishaji na utoaji elimu kwa mlipa kodi kwa njia mbalimbali,” imesema taarifa ya Kidata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!