Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika afuta maneno ya Waziri kwenye kumbukumbu za Bunge
Habari za Siasa

Spika afuta maneno ya Waziri kwenye kumbukumbu za Bunge

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson ameagiza maneno ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula dhidi ya Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi, kufutwa kwenye kumbukumbu za Bunge (Hansard). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Itakumbukwa kuwa juzi tarehe 21 Juni, 2022 bungeni hapo, Kunambi aliomba mwongozo wa Spika kuhusu maneno ya Dk. Mabula ambayo alidai yanamvunjia heshima endapo yanaruhusiwa na kama yanaruhusiwa athibitishe au afute kauli yake.

Dk. Mabula alisema kuwa mfano aliotoa mbunge huyo kuwa wakati akiwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma alisimamia vizuri upimaji wa viwanja, haufai kuwa mfano mzuri kwasababu ulikuwa wa dhuluma kwa wananchi na kuacha malalamiko mengi.

Mabula aliendelea kueleza kuwa hivi sasa Dodoma ndiyo inayoongoza kwa migogoro ya ardhi nchini ikiizidi Halmashauri ya Kinondoni ambayo ilikuwa kinara kwa muda mrefu.

Akitoa mwongozo wa suala hilo leo Alhamisi tarehe 23 Juni, 2022, Dk. Tulia alisema maneno aliyotoa Dk. Mabula dhidi ya Kunambi ni Kinyume na kanuni ya 76 ya Kanuni za kudumu za bunge na kwamba jambo hilo haliruhusiwi kwasababu linaingilia uhuru wa mawazo na majadiliano wa mbunge na inamvunjia heshima yake.

“Hayo si maneno yanayoruhusiwa katika mijadala ya bunge kwa mujibu wa kanuni ya 71 fasiri ya kwanza (i) na (j) zinazuia kumsema vibaya mbunge na matumizi yasiyo sahihi ya lugha ya kumdhalilisha mbunge,” amesema na kuendelea;

“Hivyo haikuwa sahihi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutamka kuwa ilikuwa dhuluma kwa wananchi endapo kuna dhuluma ilifanyika kuna vyombo vinavyohusika vinaweza kuchukunguza na kuchukua hatua stahiki zikachukuliwa.”

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson

Dk. Tulia amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 76 ya Kanuni za kudumu za bunge maneno hayo hayaruhusiwi na haikuwa sahihi kwa Waziri kuyatamka.

“Hivyo naelekeza maneno yanayolalamikiwa yafutwe kwenye ‘hansard’ ya tarehe 21 Juni 2022 kwa mujibu wa kanuni ya 5 fasiri ya kwanza ya Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2020,” amehitimsha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!