Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Mhagama azindua ‘Mwalimu Spesho’ ya NMB, atoa maagizo
Habari Mchanganyiko

Waziri Mhagama azindua ‘Mwalimu Spesho’ ya NMB, atoa maagizo

Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora nchini Tanzania, Jenista Mhagama ametoa rai kwa Benki ya NMB kuhakikisha inawafikia watumishi wengi zaidi kwa wakati mmoja wakiwemo walimu ili kuwasaidia kujiendeleza kimaisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo aliitoa wiki hii akizungumza na walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wa Kanda ya Kati jijini Dodoma katika siku ya Mwalimu iliyo andaliwa na NMB ikienda sambasamba na uzinduzi wa Mpango wao Maalum wa “Mwalimu Spesho.”

Siku hiyo iliyooitwa kwa jila na ‘Mwalimu Spesho’ iliandaliwa na benki hiyo na kushirikisha idadi kubwa ya walimu kwa ajili ya kuzungumzia maboresho ya mikopo na suluhisho mbalimbali zinazotolewa na beki hiyo nchini huku walimu wakipongeza huduma hizo.

Waziri Mhagama alisema mpango huo mzuri usiishie kwa walimu 5,000 badala yake angetamani uwafikie walimu wengi na watumishi ili kuwajengea uwezo hasa walimu ambao ndiyo chanzo cha kuwaandaa viongozi, wataalamu wa baadae.

Alitaka NMB kusimama na walimu wakati wote ili kuwajengea uwezo akieleza jumla ya walimu 6800 wamepandishwa madaraja hivyo ni fursa kwao kuingia kwenye mikopo kwa benki ambayo inajulikana na uendeshaji wake mzuri kuliko kukopa kwenye taasisi ambazo zinawaumiza.

“Lakini nanyi walimu, najua NMB inaweza kuwajengea uwezo, nendeni mkajishughulishe na biashara zingine huku mkiwajibika kikamilifu katika yenu, usichukue mkopo ukaanza biashara halafu ukasahau kuwajibika, hilo siyo sawa,” alisema Mhagama.

Naye Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi alisema walikusanya walimu viongozi 350 kwa ajili ya kubadilishana mawazo ili kuboresha zaidi huduma za kibenki na kujadialiana kuhusu fursa zilizopo kwa ajili ya kundu la Walimu nchini.

“Tunaamini, walimu hawa zaidi ya 350, watasaidia kupeleka elimu watakayoipata hapa kwa wenzao na hata familia zao na jamii kwa ujumla juu ya huduma nzuri zinazotolewa na benki ya NMB, lengo ni kumfganya mwalimu kuwa maisha mazuri wakati wote,” alisema Mponzi.

Wakati hayo yakijiri, wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walikuwa wakijadili fursa na umuhimu wa Benki ya NMB katika kuleta mabadiliko chanya.

Walisema, NMB ipongezwe kwa uamuzi huo huku mabenki mengine yaige mfano huo.

Wakichangia katika hotuba ya bajeti kuu, kwa nyakati tofauti wabunge hao walizungumzia namna ambavyo NMB inakuwa karibu na wananchi hasa wanyonge.

Hoja ya NMB ilianzia kwa mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Teya Ntala ambaye aliomba mabenki mengine kuiga mfano wa benki hiyo kwani imekuwa ni sehemu ya kupigiwa mfano kwa wanyonge.

Mbunge huyo alizungumzia Shilingi Bilioni 200 zilizotengwa na NMB kwa ajili ya kuwasaidia mikopo kwenye elimu kwamba kiasi hicho kinakwenda kuwabeba wanyonge kwa kiasi kikubwa.

“Hizo Sh Bil 200 si kiasi kidogo, kama benki zingine zitaweza kutenga kiasi kidogo naamini Tanzania ingekuwa na wasomi wengi na watoto wa masikini kwa mpango huu wanakwenda kupata elimu ya juu kwa sababu mfumo uliotengenezwa ni mzuri na ulipaji wake una unafuu mkubwa,” alisema Dk Ntala.

Kwa upande wake, Mbunge wa Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya alipongeza NMB kwa kuwakumbuka wajasiriamali ambayo ni sehemu ya kutoa ajira kubwa kwa vijana wa Tanzania na kujiongezea kipato.

Manyanya alisema katika jimbo lake waliamua kujenga na kubiresha soko na kuwaandaa kwa ajili ya kufanya biashara lakini akasema kuwa wengi wamekopa kwenye benki hiyo na kuongeza kipato.

Aidha, Benki ya NMB inatoa mikopo mingine ikiwemo bima ya kujikinga na majanga mbalimbali, mkopo ya pembejeyo na Mashine za kilimo, fursa za kushiriki promosheni na kujishindia zawadi mbali mbali lakini wanatoa elimu ya Kifedha kwa walimu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri alisema mikopo hiyo inakwenda kuwarahisishia maisha walimu na kuwafanya wasiwe na hofu hivyo kuwahi makazini kwani wanakuwa na uhakika wa maisha yao na familia zao lakini akaomba NMB kuja na mbinu ya kudhibiti matumizi ya kadi za ATM ili ziweze kutumiwa na walengwa halisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!