July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DC Ilala: Tutumie kondom kudhibiti magonjwa, uzazi wa mpango

Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Ng’wilabuzu Ludigija

Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Ilala (DC) jijini Dar es Salaam, Ng’wilabuzu Ludigija ameishauri jamii kutumia kondom ili kudhibiti mimba zisizotarajiwa pamoja ya magonjwa ya maambukizi ikiwemo Ukimwi. Anaripoti Mary Victor, Dar es Salaam … (endelea).

Ludigija aliyasema hayo katika uzinduzi wa bidhaa ya Lifeguard kondom uliofanyika jijini humo hivi karibuni.

Ludigija alisema, “kondom ni bidhaa inayoweza kutafsiriwa inatumika katika mambo yasiyo mema, hasa kwa tukio la kingono lakini inayo umuhimu mkubwa kwa jamii hasa katika kupambana na uzazi wa mpango kwa wanandoa kwa sababu tunaweza kudhibiti mimba zisizotarajiwa hata kuwa na uzazi wa mpango kwa kutumia kondom.”

“Pamoja na hayo kondom pia imekuwa nyenzo kubwa inayosaidia uzazi wa mpango kama ambavyo nimetangulia kusema, ni muhimu sana sisi Watanzania na wana Dar es Salaam kwa maana hasa kwa tukio hili linafanyika kwenye mkoa wetu wa Dar es Salaam na kwenye Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tutajenga utamaduni wa matumizi sahihi ya condom ili kuweza kusaidia kupanga familia zetu ili kuweza kupunguza umaskini kwa kuwa familia unayoweza kuihudumia,” amesema.

“Kondom ni moja ya nyenzo inayoweza kutumika katika suala zima la kupanga uzazi kutoka mtoto mmoja hadi mtoto mwingine,.”

“Pia tumeweza kushuhudia kwenye jamii zetu mpaka kwenye nchi za nyanda za juu kwenye nchi za Kusini lakaini hata hapa Dar es Salaam maambukizi yamekuwa ni makubwa sana hususani vijana wenye umri chini ya miaka 40,” amesema.

Kwa mujibu Ludigija upatikanaji wa bidhaa ya kondom inayotolewa na Marie Stopes; “Tungetamani sana iweze kusambazwa kwa ukubwa wake katika maeneo ya pembezoni lakini kwenye miji yenye mzunguko wa kibiashara ili kuhakikisha tunawalinda vijana wetu kwa kujikinga na maambukizi mapya ya Ukimwi ili kuhakikisha tunakuwa na taifa lenye nguvu kazi ya kesho.”

“Nitoe wito kwa vijana kukumbuka matumizi sahihi ya kondom kwani ni njia mojawapo ya kujihakikishia usalama na kufikia malengo waliyo nayo.”

Alisema kama inavyofahamika chagamoto ya mimba ambazo kwa sasa zinafikia asilimia 4, ni kubwa sana kwa vijana walio chini ya miaka 20 na pia kwa mujibu wa takwimu ziizopo maambukizi ya Ukimwi hasa miongoni mwa vijana ni kubwa hasa kwa wale walio na umri wa miaka 15 na 24

“Ninyi wenyewe ni mashahidi na kwa mujibu wa takwimu za wizara yetu ya afya zimekuwa zikitolewa, tunatamani sana vijana walioko sekondari, vyuoni kama serikali hatuungi mkono kufanya ngono za aina yoyote lakini tunajua wanachofikia ule umri wa ngono,” alisema

Alisema ni suala ambalo liko wazi na sisi kama serikali tunaendelea pia kutoa wito kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki kuendelea kutoa elimu kwa watoto ili wajue kwamba matumizi ya condom isitafsiriwe kwa njia moja au nyingine kwamba ni uasherati na hasa pia kwa taasisi za kidini, tunavyoongelea kondom hatumaanishi serikali pengine tunahamasisha zaidi ngono, lakini lengo kubwa ambalo tunalifanya kama serikali ni kwamba tunakilinda kizazi kijacho juu ya maambukizi mapya ya Ukimwi

“Ukweli usiopingika kwamba ngono inafanyika kwa vijana wetu kutokana na umri wao na vichocheo walivyo navyo katika miili yao. Kwa hiyo kondom ya Lifeguard imekuja kuongeza tija katika mapambano dhidi ya changamoto hizi ambazo nasi kama serikali tunazifanyia kazi,” alisema.

Mkurugenzi wa MarieStopes Tanzania, Vadacanthra Chandrashekar

Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa MarieStopes Tanzania, Vadacanthra Chandrashekar alisema uwepo wa kondom nchini umeweza kudhibiti mimba zisitarajhiwa milioni 1.4 ambazo zimewezesha kuokoa maisha ya wajawazito 2,800 mwaka jana.

Alisema, “MST imeendelea kufanya kazi kwa ushirikiano wa serikali ili kuboresha mifumo ya afya nchini kwa kuhakikisha wanawake walio wengi wanapata huduma bora za afya.

“Huduma zetu nyingi tunazotoa zinatolewa katika vituo vya afya vya umma katika mikoa yote nchini, mwaka 2021 timu yetu ilienda katika vituo vya afya vya umma zaidi ya 5,000 kutoa sindano,vipandikizi na huduma nyinginezo,” alisema

Alisema, “uzinduzi wa bidhaa mpya ya uzazi wa mpango wa Lifeguard ni ishara nzuri ambayo itawapa wateja bidhaa ambazo zitawezesha kudhibiti maisha yao.

“Tunafanya kazi na serikali na washirika wengine kuhimiza matumizi ya vidhibiti mimba, tunaleta bidhaa za kusisimua zaidi ili wanawake, wasichana waweze kutimiza mahitaji yao ya uzazi.

“Lifeguard kondom ni bidhaa ya pili kuzinduliwa na MarieStopes baada ya bidhaa za Misoprostol kuingia sokoni kutokea nchi jirani,” alisema

error: Content is protected !!