Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bunge la Tanzania laahirishwa ghafla
Habari Mchanganyiko

Bunge la Tanzania laahirishwa ghafla

Spread the love

BUNGE la Tanzania limeahirishwa kwa dharura leo Alhamisi tarehe 2 Juni 2022 kwa muda wa nusu saa kuanzia saa 4:00 asubuhi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mwenyekiti wa Bunge, David Kihenzile ameahirisha Bunge hilo wakati Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Catherine Magine akianza kuchangia bajeti ya wizara ya nishati na madini kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Wakati Magige akianza kuchangia, kuna sauti ya mbunge imesikika ikiomba mwongozo wa kiti cha spika na hakupewa nafasi lakini alikuwa akihoji kutokuwepo kwa mawaziri wa wizara hiyo, January Makamba na naibu wake, Stephen Byabato.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa Bunge, Kihenzile amesema, Serikali ipo hivyo akimtaka Magige kuendelea kuchangia.

Jambo hilo liliibua kidogo minong’ono na alionekana makatibu wa Bunge wakitoka walipokuwa wamekaa kwenda kwa mwenyekiti wa bunge kama mara mbili hivyo na baada ya sekundi kadhaa, Kihenzile akatangaza kuahirisha Bunge kwa dakika 30.

Baada ya muda huo wa nusu saa kumalizika, Bunge lilirejea baada ya mawaziri Makamba na naibu wake, Byabato kufika. Haijafahamika walichelewa wapi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!