MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya imeshauri pande zinazokidhana ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheni Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde kudumisha amani wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).
Ushauri huo umetolewa leo Jumatano, tarehe 01 Juni 2022 na Jaji James Karayemaha mara baada ya kumaliza kusikiliza hoja za pande mbili zinazovutana kuhusu uongozi.
Amesema kila upande una wajibu wa kuleta amani wakati wakisubiri mahakama kutoa maamuzi juu ya mgogoro huo.
Jaji Karayemaha amesema ni vema kila upande uendelee kudumisha amani kama maagizo ya dini yanavyotaka.
Aidha, amewataka kukwepa kuingia mikononi mwa Jeshi la Polisi ili kuendelea kumsaidia Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kudumisha amani na kufanya shughuli za kuleta maendeleo.
Jaji huyo ametoa ushauri huo wakati akiahirisha kusikiliza kesi hiyo hadi tarehe 3 Juni 2022saa tano asubuhi kwa ajili ya kutoa uamuzi wa shauri hilo.
Ni kesi namba 3/2022 na kesi namba 14/2022 ambazo zilizhirishwa tarehe 31 Mei 2022 ili kupisha majadiliano yaliyokuwa yakiendelea baina ya Serikali na pande zinazotofautinaa.
Upande wa mleta maombi Askofu Edward Mwaikali umewakilishwa na na Wakili William Mashoke, Samson Mbamba na Godwin Mwapongo.
Wakili wa wajibu maombi wakiongozwa na Dk. Pallangyo ameiambia mahakama kwamba wakili Azael Mwaiteni na Benjamin Mbembela wameamua kujiondoka kwenye shauri hilo na kwamba watakuja endapo Mahakama itawahitaji.
Baada ya kujiondoa mawakili wote wawili, Mahakama iliendelea kusikiliza mashauri yote mawili kesi namba tatu ya mwaka 2022 na kesi namba 14 ya mwaka 2022.
Shauri la kwanza ambalo lililetwa na mleta maombi ni kupinga kuondolewa madarakani, kutakiwa kurejesha vitendea kazi vya uaskofu na shauri la pili kuzuia uapisho wawajibu maombi namba nne na namba tano.
Wakili Dk Pallangyo aliiambia Mahakama kuwa hoja zililetwa na mleta maombi hazina mashiko na pia Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi sababu sula hilo ni lakidini na kiimani.
Kutokana na hoja Wakili Pallangyo, aliiomba Mahakama kutupilia mbali hoja za mleta maombi sambamba na kulipa gharama za kesi.
Kwa upande wa Wakili wa mleta maombi, Samson Mbamba, ameiambia mahakama utaratibu uliotumika kufanya mkutano mkuu, 22 Machi 2022 na kumchagua mjibu maombi namba nne na tano haukuwa halali kwa mujibu wa katiba ya KKKT Dayosisi ya Konde, kifungu namba 13 ya mwaka 2015.
Akirejea baadhi ya kesi ambazo shughuli zote zilizohusu taasisi zilisitishwa wakati kesi ya msingi ikiendelea mahakamani, hivyo kutolewe zuio la kusitishwa kwa shughuli za uapisho na kukabidhi ofisi na vifaa vyote vya kiuaskofu.

Katika hoja hiyo wakili, Godwin Mwapongo aliiambia mahakama kuwa hali hiyo imeleta mkanganyiko baina ya pande zote mbili na kusababisha baadhi ya waumini kufunguliwa kesi za jinai namba 45 na 46 ya mwaka 2022 kwenye kanisa la KKKT Matema.
Wakili Mwapongo akasema zuio la uapisho litasaidia kuleta amani na kutoa nafasi kwa kesi ya msingi kusikilizwa mahakamani badala ya upande wa mjibu maombi kuendelea na shughuli za uapisho zinazotarajiwa kufanyika tarehe 3 Juni 2022.
Hata hivyo, akaiomba mahakama kwamba kila upande ubebeb gharama zake za uendeshaji wa kesi mahakamani hapo.
Akizungumzia hoja hizo Wakili wa upande wa mjibu maombi, Peter Kilanga, ameiambia mahakama kwamba hoja za upande wa mleta maombi hazina mashiko kwa sababu shughuli zote za kidayosisi zinaendelea na kinachosubiriwa ni uapisho ambao unampa mamlaka mjibu maombi namba nne na tano kuendelea na kazi.
Kutokana na hali hiyo, wakili Kilanga akaiomba mahakama hoja za mleta maombi zitupiliwe mbali kwa sababu hazina mashiko sambamba na kulipa gharama zote uendeshaji kesi.
Kiongozi wa kuchaguliwa wa Kanisa unapopata upinzani jirekebishe usamehewe. Unapojifanya eti una madaraka na kwamba ukae hadi muda wako uishe bila kujali malalamiko ndo unaleta haya matatizo.
Kung’ang’ania madaraka ya kuchaguliwa ni dalili za kufilisika katika uongozi wako.