September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Ndugulile aendelea ‘kulilia’ vivuko Kigamboni

Kivuko cha Magogoni

Spread the love

 

MBUNGE wa Kigamboni jijini Dar es Salaam kupitia chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Faustine Ndugulile amesema, kilio cha ubovu wa vivuko kwa wananchi wa Kigamboni ni cha muda mrefu na jitihada za haraka zinahitajika kufanyika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Ndugulile kwa kipindi kirefu amekuwa akizungumzia kero hiyo ambayo inasababishwa na vivuko hivyo kutoa huduma kwa kusuasua kwa baadhi kuharibika hivyo kusababusha adha kwa wananchi.

Hivi karibuni, akiwa bungeni jijini Dodoma alishauri kama Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imeshindwa kuvisimamia ivibinafsishwe.

Dk. Faustin Ndungulile, Mbunge wa Kigamboni

Leo Alhamisi tarehe 2 Juni 2022, ametumia ukurasa wa kijamii wa Twitter kuweka picha ya kivuko na umati wa wananchi huku akiandika, “hatua za haraka zinahitajika kunusuru hali hii.”

“Tusisubiri maafa halafu tuunde Tume. Kama TEMESA imeshindwa, huduma hii ibinafsishwe. Wana Kigamboni wanastahili huduma bora, salama na ya uhakika ya vivuko. Ni haki na sio hisani.”

error: Content is protected !!