WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda, amesema marekebisho ya sera ya elimu na mitaala, yatakamilika Desemba 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Prof. Mkenda ametoa taarifa hiyo katika sherehe za kilele cha wiki ya ubunifu kitaifa, zilizofanyika leo Alhamisi, tarehe 19 Mei 2022, jijini Dodoma.
Waziri huyo wa elimu amesema, hadi itakapofika Septemba 2022, taarifa kuhusu mabadiliko hayo zitafikishwa kwa viongozi wakuu wa nchi.
“Katibu Mkuu wa UN ameita kikao cha wakuu wa nchi jijini New York, Marekani Septemba mwaka huu kuzungumzia masuala haya ya mageuzi katika elimu. Bahati nzuri sisi tumeshatangulia kwa sababu Rais wetu alishatuelekeza kufanya kazi hiyo. Nadhani itakapofika Septemba tutakuwa tumeshatoa briefings kwa wakuu wa nchi,” amesema Prof. Mkenda na kuongeza:
“Tuko tayari kukamilisha kazi yote tukifika Desemba ili mwakani wakati dunia inafanya mchakato sisi tumeshafanya maamuzi.”
Leave a comment