Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Kigwangalla ataka mabadiliko mgawanyo wa ajira
HabariHabari Mchanganyiko

Kigwangalla ataka mabadiliko mgawanyo wa ajira

Spread the love

MBUNGE wa Nzega Vijijini, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), ameishauri Serikali ibadili mfumo wa utoaji ajira za watumishi wa umma, akitaka iajiri watu kutoka maeneo yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora…(endelea).

Dk. Kigwangalla ametoa ushauri huo leo Alhamisi, tarehe 19 Mei 2022, akizungumza katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan, mkoani Tabora.

Mbunge huyo wa Nzega Vijijini, ametoa ushauri huo akizungumzia ajira zilizotangazwa na Serikali hivi karibuni, zaidi ya 10,000.

“Tunafahamu utaratibu wa kawaida watoto wataajiriwa central halafu watasambazwa kwenye maeneo yenye uhitaji nchi nzima. Sisi tunaomba kuwe na usawa kwenye kugawa nafasi za ajira wachaguliwe kutoka katika eneo wanalotoka katika majimbo yao,” amesema Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla amesema “kama ambavyo mmetugawia pesa za barabara kwenye kila jimbo, basi hivyo hivyo na nafasi za ajira zigawanywe kwa usawa kutokana na vigezo mbalimbali ambavyo Serikali haitashindwa kuweka.”

Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameiomba Serikali ikamilishe ujenzi wa miradi ya maendeleo, iliyoanza kujengwa jimboni mwake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!