Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kasekenya awataka makandarasi kuwajibika kifikra
Habari Mchanganyiko

Kasekenya awataka makandarasi kuwajibika kifikra

Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka makandarasi, waajiri na wasimamizi wa mradi kuwa na ushirikiano mzuri ili kuwezesha miradi ya ujenzi inayofanyika nchini kuwa ya viwango bora. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akifunga mkutano wa siku mbili wa mwaka wa mashauriano wa makandarasi jijini Dodoma leo tarehe 14 Mei, 2022 Mhandisi Kasekenya amewataka makandarasi kuwa waadilifu na wanaofanya kazi kwa weledi ili miradi inayojengwa nchini iwiane na thamani ya fedha.

“Kumbukeni kuwa kila haki ina wajibu hivyo mkitekeleza wajibu wenu kikamilifu mtawawezesha waajiri kuwapa haki zenu kwa wakati,” amesema

Amezungumzia umuhimu wa makandarasi kushirikiana na wataalamu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), ili kupata taarifa sahihi kabla ya utekelezaji wa miradi yao.

Kasekenya amewaahidi makandarasi kuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi itafanyia kazi maazimio yao yote ili kuhakikisha changamoto za makandarasi na wadau wengine wa ujenzi zinapatiwa ufumbuzi.

“Wajibikeni kifikra ili miradi yenu mnayoitekeleza iwe ya viwango bora na hivyo kuwatendea haki watanzania na kukuza sekta ya makandarasi hapa nchini”, amesema Naibu Waziri Kasekeya.

Naye, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Rhoben Nkori, amezungumzia umuhimu wa waajiri kuheshimu mikataba ya kazi ili kuleta haki, kuepuka vitendo vya kudhalilisha makandarasi wawapo kazini na kutoa fursa kwa makandarasi wazawa katika miradi ili kuwajengea uwezo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya

Zaidi ya washiriki 860 wakiwemo makandarasi, wataalam washauri na wadau wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni wameshiriki mkutano huo uliolenga kutathimini umuhimu na mchango wa makandarasi katika uchumi wa Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!