Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwandishi wa habari afariki baada ya kujifungua
Habari Mchanganyiko

Mwandishi wa habari afariki baada ya kujifungua

Marehemu Hannerole Mrosso
Spread the love

 

CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (MBPC) kimepata pigo baada ya kuondokewa na mwanachama wake wa muda mrefu, Hannerole Mrosso aliyefariki baada ya kujifungua katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kitengo cha Wazazi Meta Jijini Mbeya tarehe Mei, 2022. Anaripoti Kenneth Ngelesi, Mbeya … (endelea).

Akitoa taarifa mume wa marehemu Baraka Kasubiri ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii amesema mkewe alifanyiwa upasuaji na kujifungua mtoto wa kike na muda mfupi baada ya kujifungua alipoteza maisha.

Taratibu za mazishi zinafanywa eneo la Sokomatola Jijini Mbeya ambapo mwili utasafirishwa kwenda Namtumbo Mkoani Ruvuma kwa maziko yanayotarajiwa kufanyika tarehe 15 Mei, 2022.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Joseph Mwaisango amesema marehemu alikuwa ni mwanachama ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa tasnia ya habari pia alikuwa na ushirikiano na kila mtu.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uchumi kwa wanahabari (MJEF), Kakuru Msimu amesema msiba huu umewaumiza hasa pale ambapo wanapompoteza mwenzao ambaye walitegemea kujikwaamua kiuchumi.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wanahabari wanawake, Esther Macha amesema wamepata pigo kwani wamempoteza mwanachama wao ambaye alikuwa na mchango mkubwa tangu kuanzishwa chama chao.

Sambo amesema marehemu ambaye pia alikuwa mwanachama chama cha kusaidiana wanahabari (Amani) amefariki wakati chama chao kikiwa kichanga na marehemu alikuwa mshiriki mwaminifu.

“Ni vigumu kuamini kuwa Hannerole ametuacha kwani upole wake na ucheshi wake ulikuwa ni faraja katika kikundi” amesema Martha.

Naye mwandishi mwandamizi Felix Mwakyembe amesema tasnia imeondokewa na mwandishi ambaye alipenda kujifunza na kujiendeleza kielimu ambapo hadi umauti alikuwa akisoma Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) Mbeya.

Mmoja wa wanafunzi wa TEKU Shaban Nassoro Kisilwa amesema ndoto za mwenzao zimezimika ghafla kwani walitarajia kuhitimu naye mwaka huu.

Shughuli zote za msiba zinaratibiwa na Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Kenneth Mwakandyali ambapo amewataka waandishi kushirikiana katika kumsindikiza mwenzao katika safari yake ya mwisho.

Enzi za uhai wake marehemu amewahi kuhudumu kituo cha Radio cha Generation Fm na Baraka Fm akiwa masomoni.

Marehemu ameacha watoto watatu wawili wakiwa ni mapacha Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!