Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Wanaoguswa ripoti ya CAG wanachukuliwa hatua
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Wanaoguswa ripoti ya CAG wanachukuliwa hatua

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake inawachukulia hatua watu wanaotajwa kufanya ubadhirifu katika ripoti za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha Azam, yaliyorushwa leo Jumatano, tarehe 4 Mei 2022, Rais Samia amesema, Serikali huwa inafanyika kazi mapendekezo ya ripoti ya CAG, lakini haitangazi hadharani ndiyo maana wananchi hawajui hatua zinazochukuliwa.

“Kinachotokea ni kwamba, CAG anavyomalizia ripoti yake anatakiwa kuikabidhi kwa Rais, na Rais haraka anatakiwa kuikabidhi bungeni na ikifika bungeni inajadiliwa. Kawaida hoja za CAG akishakuletea serikalini, Serikali inakaa na kupitia hoja baada ya hoja. Zinazotolewa nyingi zina majibu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “kwa hiyo tunapojibu hatujibu kwenye kamera, tunajibishana baina ya sisi na CAG, tunamwambia hili tumeshalifanyia kazi, anakuja kutizama ni ukweli anaweka tiki.”

Mkuu huyo wa nchi amesema, Serikali ilifanyia kazi ripoti ya CAG ya 2019/2020, kwa kuwachukulia hatua wahusika, ikiwemo baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), waliotajwa kuhusika katika ubadhirifu.

2 Comments

  • Kwanini serikali “haitangazi hadharani” ? Inaogopa nini? Wezi, wabadhirifu na wala rushwa wanachukuliwa hatua bila wananchi kujua? Wananchi hawahusiki? Du hii ni ya mwaka. Mama tuambie ukweli yakhe tafadhali

  • Asante wezi wa Mali ya umma inatakiwa wanaoubiwa waelewe hatua gani walizo chukiliwa wezi hao sasa ukiwa wanchukuliwa hatua za siri walio ibiiwa ni umma wa kiitanzania usijue kweli haki haki io alioibiwa asijue hukumu ya mwizi wake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!