May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo chashauri Serikali iondoe tozo za Sh 500 kwenye mafuta

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeishauri Serikali iondoe tozo ya Sh. 500 kwa kila lita ya mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya taa, ili kupunguza makali ya mfumuko wa bei uliosababishwa na kupanda kwa nishati hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatano, tarehe 4 Mei 2022, na wasemaji wa kisekta wa chama hicho, Isihaka Mchinjita (Sekta ya Madini), Emmanuel Mvula (Sekta ya Fedha na Uchumi) na Ally Salem ( Sekta ya Habari, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi).

“Mapendekezo yetu Serikali isimamishe kwa muda angalau tozo ya Shilingi 500 kwenye mafuta. Katika kila lita ya Petroli, Diseli na Mafuta ya taa Serikali isimamishe kuchukua Sh. 500 ili kukabiliana kupaa kwa bei,”imesema taarifa hiyo

Chama hicho kimeishauri Serikali kutumia fedha zake za akiba, ili kuziba pengo endapo itaondoa tozo hiyo, huku ikiishauri iongeze uwezo wa kuagiza mafuta ili kuwa na akiba yake nchini.

Taarifa ya chama hicho imeeleza kuwa, ongezeko la bei ya mafuta linawapa mzigo wananchi kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu.

“Jana Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa, huku tukiona ongezeko la bei za rejareja za petroli kwa Sh. 287 sawa na 10%, Dizeli Sh. 566 kwa kila lita sawa na asilimia 21% na Mafuta ya taa Sh. 430 sawa na 16.03% kwa kulinganisha na bei za mwezi April,”

Taarifa hiyo imesema “na kufanya bei mpya ya Petroli kuwa Sh. 3,148 kutoka 2,861, kwa Dar es Salaam na bei ya juu zaidi kuwa 3,495, Kagera kwa Tanzania Bara. Bei ya Diseli ni Sh. 3,258 kutoka Sh. 2,692 na bei ya mafuta ya taa Sh. 3,112 kutoka Sh. 2,682. Bei hizi zimetangazwa kuanza kutumika leo.”

error: Content is protected !!