May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Wanaoguswa ripoti ya CAG wanachukuliwa hatua

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake inawachukulia hatua watu wanaotajwa kufanya ubadhirifu katika ripoti za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha Azam, yaliyorushwa leo Jumatano, tarehe 4 Mei 2022, Rais Samia amesema, Serikali huwa inafanyika kazi mapendekezo ya ripoti ya CAG, lakini haitangazi hadharani ndiyo maana wananchi hawajui hatua zinazochukuliwa.

“Kinachotokea ni kwamba, CAG anavyomalizia ripoti yake anatakiwa kuikabidhi kwa Rais, na Rais haraka anatakiwa kuikabidhi bungeni na ikifika bungeni inajadiliwa. Kawaida hoja za CAG akishakuletea serikalini, Serikali inakaa na kupitia hoja baada ya hoja. Zinazotolewa nyingi zina majibu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “kwa hiyo tunapojibu hatujibu kwenye kamera, tunajibishana baina ya sisi na CAG, tunamwambia hili tumeshalifanyia kazi, anakuja kutizama ni ukweli anaweka tiki.”

Mkuu huyo wa nchi amesema, Serikali ilifanyia kazi ripoti ya CAG ya 2019/2020, kwa kuwachukulia hatua wahusika, ikiwemo baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), waliotajwa kuhusika katika ubadhirifu.

error: Content is protected !!