MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina ameliomba Bunge kuunda kamati ya kiuchunguzi ili kujua sababu ya Kamati ya Majadiliano ya Kesi ya Makinikia kukubali kupokea Sh 692 Bilioni tofauti na ushauri wa Mahakama ambazo zilisema Serikali inaweza kupata Sh. 6.5 trilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Mpina ametoa hoja hiyo leo Alhamisi tarehe 28, 2022 wakati akichangia majadiliano ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa bungeni.
“Mahakama za bodi za rufaa za kodi pamoja na bazara zilisema Trlioni 5.65 zinaweza kupatikana kama kodi lakini kwanini tupate Bilioni 692, ningeomba eneo hili linachangamoto na ningeshauri bunge liunde Tume Teule ya Bunge iende ikachunguze hili kwanza negotuon timu ilifikiaje maamuzi ya kupokea fedha hizo na uhalali wa majadiliano hayo n akile kilichopatikana
Alisema ukiondoa kesi za makinia kuna kesi za Sh Trilioni 5.19 za makosa mbalimbali na kwamba sasa hivi rufaa za kodi zinafikia Trlioni 2 kwa mwaka.
“Tukiruhusu haya kila siku wafanyanbiashara watakuwa wanatukatia rufaa na tutakuwa tunakosa fedha kama kesi hazisikilizwi kwasababu mabaraza hayana fedha au hayana watumishi ni jambo ambalo hakliingii akilini,” amesema Mpina.
Mpina amezungumzia pia namna usiri wa mikataba unavyoligharimu Tauifa akitolea mfano wa Mkataba wa ujenzi wa Bwawa la Umeme wa Julius Nyerere.
Amesema maeneo hayo yana changamoto nyingi ndiyo maana taasisi za uchunguzi zimekuwa zikiibua ubadhirifu mara kwa mara.
“Katika utekelezaji tumetangaziwa utamalizika baada ya miaka miwili ijayo lakini ndani ya mkataba ipo clear kuna bilioni 260 za CSR, na mkandarasi akichelewesha mkataba kwa mwaka mmoja anailipa Serikali asilimia 10. Sasa amechelewesha kwa miaka miwili tunamdai Sh 1.3 trilioni za kuchelewesha mkataba kwa miaka miwili kwanini kuna usiri?” amehoji Mpina.
Leave a comment