Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko GF TRUCKS yafuturisha wadau na wafanyakazi, yatoa ujumbe
Habari Mchanganyiko

GF TRUCKS yafuturisha wadau na wafanyakazi, yatoa ujumbe

Spread the love

 

WAISLAMU na wanajamii kwa ujumla wametakiwa kuutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kubadili tabia kwa kutenda yaliyo mema na kuyaendeleza hata baada ya kumalizika mfungo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni GF Truck & Equipments LTD, Mehboob Karmali jana Jumatano tarehe 27 Aprili 2022 mara baada ya kufuturisha wadau mbalimbali na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Alisema mara nyingi mwezi huo umekuwa ukileta utulivu katika jamii, “haijalishi ni kijana, mzee, Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu, ilimradi wengi hutulia na kuuheshimu, hivyo ni vema kuendeleza yale mema hata katika nyakati nyingine ili jamii iwe salama.”

“Kipindi hiki pia ni vema kuwapa wahitaji sadaka kwa kile kidogo tutakachojaaliwa kwa sababu tunazidiana,“ alisema Karmali.

Kwa upande wake, mgeni mualikwa katika Iftari hiyo, Sheikh wa msikiti wa Khoja Shia Ishnashri Jamaat ya nchini Marekani, Syed Ali Raza Rizvi aliwasihi Waislamu hususani vijana kudumisha amani na upendo baina yao.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaasa wafanyakazi wa kampuni hiyo kufanya kazi huku wakimtanguliza Mungu ili wanapofanya maamuzi yoyote yawe kwa faida ya kazi yao na Taifa kwa ujumla.

“Ukimtanguliza Mungu katika kila jambo lazima utafanikiwa, ila ukiwajali wengine na kuwahurumia utafanya maamuzi ya busara siku zote, hivyo tuyazingatie haya ili kufikia mafanikio tunayoyakusudia,” alisema Raza Rizvi.

Alisema hii ni kawaida kampuni ya GF Trucks & Equipemnts LTD, kujumuia na wafanyakazi wake na wadau katika matukio mbalimbali ikiwamo kufuturisha pamoja na kutoa misaada kwa yatima na wasiojiweza.

Kampuni hiyo inajishungulisha na uuzaji wa magari makubwa(trucks) na mitambo yakutengenezea barabara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!