Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yapanda kwa nafasi saba hali ya rushwa
Habari Mchanganyiko

Tanzania yapanda kwa nafasi saba hali ya rushwa

Salumu Hamduni, Mkurugezni Mkuu wa TAKUKURU
Spread the love

TANZANIA imepanda imepanda kwa nafasi 7 katika vipimo vya nchi zenye rushwa kutoka nafasi ya 94 mwaka 2020 hadi nafasi ya 87 mwaka 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi tarehe 21 Aprili, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama, wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya bajeti ya mwaka 2022/23.

Mhagama amesema takwimu hizo ni kwa mujibu wa taarifa ya Transparency International ya mwaka 2021 iliyotoka Februari, 2022.

Amesema kupitia Kiashiria cha Corruption Perception Index inaonesha kuwa Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwa kupata alama 39 na kushika nafasi ya 87 kati ya nchi 180.

“Kwa mafanikio haya Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti wa World Justice Project (WJP) unayotumia kiashiria cha “The Rule of Law Index” unaonesha kuwa kwa mwaka 2020, Tanzania iliendelea kufanya vizuri kwa mwaka wa pili mfululizo katika kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka kwenye mihimili ya utawala, mahakama na bunge.

Amesema katika utafiti huo Tanzania imeshika nafasi ya 93 kati ya nchi 128 duniani, ikiwa ni nchi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki na nafasi ya 13 kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Vilevile amesema kwa mujibu wa utafiti wa taasisi binafsi ya Research on Poverty Alleviation (REPOA), uliotolewa mwaka 2022 unaonesha kuwa Tanzania inafanya vizuri katika kulikabili tatizo la rushwa na kuwa imepungua katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

1 Comment

  • Je, hichi ni kipindi cha awamu ya tano?
    Tumeshashuka uchumi kwa sababu ya uwizi na rushwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!