Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Biashara Serikali yasema bei ya bidhaa Tanzania zipo chini
BiasharaTangulizi

Serikali yasema bei ya bidhaa Tanzania zipo chini

Spread the love

LICHA ya kuwepo kwa mfumuko wa bei za bidhaa duniani Serikali ya Tanzania imesema bei za bidhaa nchini mwake zipo chini ikilinganishwa na nchi zingine za Afrika Mashariki. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yamelezwa leo Jumatato tarehe 11 Aprili, 2022 na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mwenendo wa bei nchini.

Dk. Kijaji ametaja baadhi ya bidhaa ambazo bei zake zipo chini ikilinganishwa na wastani wa bei wa nchi zingine za Afrika Mashariki.

Amesema wastani wa bei ya saruji kwa nchi zingine za Afrika Mashariki ni Sh 16,527 kwa mfuko wa kilo 50 huku Tanzania ikiwa ni Sh.16,125, “na tunaamini tunapoendelea kukaa na kuzungumza bei hiyo inaweza kushuka zaidi.”

Amesema bei ya petrol kwa nchi zingine za Afrika Mashariki ni Sh 2,971 kwa lita huku Tanzania ikiwa ni Sh 2,616 kwa bei za mwezi Machi.

“Unga wa ngano nchi zingine ni Sh 1,886 sisi ni 1,735, sukari ni Sh 3,034 sisi ni 2,670,” amesema Dk. Kijaji.

Kwa upande wa vifaa vya ujenzi amesema kwa nchi zingine kwa mabati ya geji 30 ni Sh 24,978 wakati Tanzania ni Sh 21,952.

Kwa upande wa nondo za 12mm amesema wakati nchi zingine ni Sh 42,113, nchini Tanzania zinapatikana kwa Sh 25,911 tu.

hata hivyo Dk. Kijaji amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua zaidi kuhakikisha bei zinapungua ikiwemo Mamlaka na taasisi husika kusimamia mienendo ya bei za bidhaa bila kuumiza uapande wowote.

Pia kufanya vikao kazi na wadau wa uzalishaji ili kuhakikisha mbutuko wa uchumi wa ndani unatafutiwa ufumbuzi, kuanzisha mfumo wa upatikanaji wa bei za bidhaa mbalimbali kila siku na kituo cha mawasilinao kwa wananchi kuwasilisha maoni kuhusu bei katikamaeneo yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

error: Content is protected !!