Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ujenzi Kituo cha Afya waneemesha mafundi ujenzi Mtama
Habari Mchanganyiko

Ujenzi Kituo cha Afya waneemesha mafundi ujenzi Mtama

Spread the love

UJENZI wa Kituo cha Afya Mtama mkoani Lindi umetajwa kuwa kichocheo cha maendeleo kwa wakazi wa eneo hilo hususani mafundi ujenzi ambao wameshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mradi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Shodadi Katuya (32) mzaliwa wa Mtama ambaye pia ni fundi ujenzi aliyehitimu Chuo cha Ufundi Ndanda.

Amemshukuru Rais Samia kwa kupeleka mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya kwa kuwa yeye ni kati ya vijana walionufaika na mradi huo kwa kushiriki katika ujenzi wake.

Amesema mradi huo umefungua ajira nyingi kwa vijana na akina mama wanaotoa huduma ya chakula maarufu kama ‘mama ntilie.’

“Kuna vijana wengi wameacha kuzurura mtaani wako hapa wametengeneza ajira zao kama ulivyoona huko nje.

“Pia imewakomboa watu katika mambo mengi hususani katika kipindi hiki cha kilimo, watu wameacha kutumia jembe la mkono wamechukua hela yake ya kibarua hapa wameenda kuweka kule kwenye matreka wamelima heka tatu, heka nne heka tano na anaendelea… hayo yote ni kutokana na kipato walichopata hapa,”amesema Shodadi.

Aidha, Shodadi amesema kwamba zabuni aliyoipata ya ujenzi wa kituo hicho imemsaidia kununua bodaboda yake na kuendeleza maisha yake.

“Mimi mwenyewe sasa hivi namiliki bodaboda yangu binafsi kupitia tu miradi hii hapa na tunamshukuru sana mama Samia kwa sababu sekta aliyoishika hii ni sekta ya afya ambayo inamgusa kila mmoja wetu, kiasi kwamba kutuletea Mtama tunahisi kama  ametupendelea …tuna kila sababu ya kumshukuru na tunamshukuru sana tu,” amesema  Shodadi.

Aidha, akifafanua namna alivyopata zabuni ya ujenzi wa kituo hiko cha afya. Shodadi amesema aliipata kutoka kwenye Halmashauri baada ya tangazo kutoka na yeye kupeleka barua ingawa hakuwa na uhakika kama angepata kazi hiyo kwani walikuwa waombaji wengi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!