Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mbowe waishinda Serikali ya Tanzania, EACJ yatoa maagizo
Habari za SiasaTangulizi

Kina Mbowe waishinda Serikali ya Tanzania, EACJ yatoa maagizo

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) imeitaka Serikali ya Tanzania kurekebisha vifungu vya mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya 2019, vinavyokiuka mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na haki za binadamu. Anariopoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa, tarehe 25 Machi 2022 na Jopo la Majaji watano wa EACJ, akiwemo Jaji Charles Nyachae.

Ni wakati wakitoa hukumu ya kesi namba 3 ya mwaka 2020, iliyofunguliwa na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kuipinga sheria hiyo.

Kwa mujibu wa hukumu ya EACJ dhidi ya kesi hiyo, mabadiliko hayo yanakiuka vifungu vya mkataba wa EAC, ikiwemo cha 6d na 72 pamoja na haki za binadamu, demokrasia na kisiasa.

Mwenyekiti wa Chadema nchini Tanzania, Freeman Mbowe (kushoto) akiwa na Wakili John Mallya katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki jijini Arusha

Wakili wa upande wa watetezi, John Mallya akizungumza na MwanaHALISI Online, ametaja vifungu ambavyo Serikali ya Tanzania inatakiwa ivirekebishe ni kifungu cha 3,4,5 na 29, vya Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Wakili huyo amesema, kwa sasa vifungu hivyo havina nguvu na haviwezi kutumika.

“Mahakama imeamua, hii sheria ni batili, imekiuka mkataba wa EAC na kwa sababu Tanzania ni mjumbe wa jumuiya hiyo lazima sheria zake zikitungwa zioane na masharti ya mkataba wa EAC pamoja na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kujieleza,” amesema Wakili Mallya na kuongeza:

“Na mambo mengine yanayohusiana na haki za demokrasia. Kuna vifungu mahakama imesema viondolewe ili Tanzania iendelee kuwa mwanachama wa EAC.”

Kesi hiyo ilifunguliwa na viongozi wa vyama vya siasa, akiwemo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupinga sheria hiyo wakidai inampa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Wengine kwenye kesi hiyo ni, Hayati Maalim Seif Shariff Hamad, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Chama cha CHAUMMA, Hashim Rungwe.

Katika kesi hiyo, kina Mbowe walikuwa wanapinga vipengele vya sheria ya vyama vya siasa, ikiwemo kifungu kinachompa msajili wa vyama vya siasa, mamlaka ya kuingilia wakati wowote shughuli za chama cha siasa.

Vifungu vingine vilivyopingwa ni kile kinachompa msajili wa vyama vya siasa, mamlaka ya kuingilia uongozi wa chama cha siasa na kumsimamisha uanachama mwanachama yeyote kushiriki shughuli za kisiasa.

Walidai Vifungu vyote hivyo vinakiuka misingi ya utawala bora na kidemokrasia, pamoja na mkataba wa EAC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

error: Content is protected !!