Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Katibu Mkuu Madini atembelea GGML, aipongeza kwa kuzingatia sheria
Habari Mchanganyiko

Katibu Mkuu Madini atembelea GGML, aipongeza kwa kuzingatia sheria

Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti anayesimamia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo (katikati), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolph Nduguru kuhusu shughuli mbalimbali za GGML.
Spread the love

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolph Ndunguru ameipongeza Kampuni ya (GGML) kwa kuzingatia sheria zinazosimamia sekta ya madini na kutekeleza majukumu yake kwa uweledi. Anaripoti Mwanduishi Wetu… (endelea).

Ndunguru ametoa kauli hiyo majuzi wakati akizungumza na Menejimenti ya GGML baada ya kufanya ziara katika kampuni hiyo kwa mara ya kwanza.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolph Nduguru (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja Madini, Gilbert Chamlonde (kulia) kuhusu shimo la wazi la Nyankanga lililokuwa likifanya kazi kati ya mwaka 1990 na 2020.

“Tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliponiteu kwenye wadhifa huu, nimesikia maoni mengi mazuri kuhusu GGML.

“Nakumbuka hivi karibuni mlipokea zawadi na tuzo nyingi kule mkoani Dar es Salaam. Tuzo hizo zilikuwa zinatambua utendaji kazi wenu kama kampuni bora ya uchimbaji madini kwa mwaka 2021.

“Ndio maana nimeona ni vyema kutembelea mgodi huu ili kuona kazi nzuri mnayoifanya,” alisema Ndunguru.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Adolph Nduguru akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya GGML.

Aidha, Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti anayesimamia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo alimshukuru Ndunguru kwa kutembelea mgodi huo.

Alieleza kuwa GGML itaendelea kuzalisha katika mazingira uendelevu kwa kulipa kodi na kuchangia programu mbalimbali za uwekezaji ndani ya jamii zinazosaidia wananchi wanaozunguka mgodi.

“Tumekuwa na changamoto nyingi katika shughuli zetu ikiwa ni pamoja na kupungua kwa madini yanayochimbwa kupitia uchimbaji wa wazi katika mgodi wa Nyankanga.

“Pia kulikuwa na ucheleweshaji wa utoaji wa vibali vya uchimbaji wa wazi Mlima wa Geita na Nyamulilima.

Tunashukuru kwamba sasa tuko katika hatua nzuri kwani uendelezaji wa miradi yote miwili ulianza mwaka 2021.

GGML pia imepata leseni na kuanza kazi ya utafiti madini katika maeneo ya vijijini yaliyopo katika mikoa ya Singida, Dodoma, Kishapu na Nzega,” alisema Shayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!