KUTOKUWA na ushirikiano miongoni mwa asktrai na maafisa wa Jeshi la Mageresha kumetajwa kama kikwazo cha kupiga hatua katika maendeleo ya jeshi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Hayo yameelezwa leo Ijumaa tarehe 25 Machi 2022 na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizindua midadi mablimbali ya jeshi la Magereza jijini Dodoma.
“Kuna tetesi nyingi nazipata inaelekea jeshi la magereza hamuongei lugha moja au hamvuiti upande mmoja wengiune wanavuta kusini wengine wanavuta kaskazini vinginevyo mngefanya hatua kubwa ya maendeleo kuliko hapa,” amesema Rais Samia.
Amesema anazo taarifa kuwa kila mtu anamchunga mwingine kwa mabaya kwa kusubiri mwingine akosee, “dumisheni umoja na msikamano jeshi lote livute upande mmoja, mkeendela kuvuta huku na huku hamtafika mbali,” amesema .
Amewakumbusha kuwa jeshi hilo si mali yao bali ni mali ya watanzania na kwamba wao wameaminwa tu kutoa huduma kwenye jeshi hilo.
“Yule ambaye atakuwa tayari kuturudisha nyuma kwaajili ya nafsi yake nasi tutakwenda naye pamoja,” amesisitiza.
Leave a comment