Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mama Janeth Magufuli atoa misaada kwa wahitaji
Habari Mchanganyiko

Mama Janeth Magufuli atoa misaada kwa wahitaji

Spread the love

 

MAMA Janeth, Mjane wa aliyekuwa Rais wa wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema, ataendeleza utamaduni waliyojiwekea yeye na marehemu mume wake wa kutoa misaada kwa wenye uhitaji wakati wa sikukuu za kidini ili kugawana na wenzao kidogo walichojaaliwa nacho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Mama Janeth ameyasema hayo leo Ijumaa, tarehe 18 Machi 2022, wakati akikabidhi misaada mbalimbali kwa kaya 100 zenye uhitaji, wafungwa, pamoja na watoto yatima katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita.

Amesema ameamua kutoa misaada hiyo katika kipindi hiki ambapo waumini wa dini ya Kikristo duniani kote wako katika mfungo wa Kwaresima wa siku 40 ikiwa ni ishara ya kushiriki mateso pamoja na Yesu Kristo, aliyejitoa sadaka kuteswa, kufa msalabani na baada ya siku tatu akafufuka ili kumkomboa mwanadamu.

“Kipindi cha Kwaresima ni cha kufunga na kufanya toba. kutafakari maisha yetu, tujikane nafsi zetu kwa kutenda matendo mema na kujizuia kutenda vitendo viovu ili kujisogeza karibu na Mwenyezi Mungu,” amesema.

“Katika kipindi hiki tunaaswa kusaidia wenye uhitaji na shida mbalimbali kwani (Mithali 19:17) Amhurumiaye masikini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema,” amesema Mama Janeth

Misaada hiyo ameitoa ikiwa ni siku moja baada ya kuadhimisha kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Hayati Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, jijini Dar es Salaam na mwili wake kuzikwa nyumbani kwao Chato.

Kumbukizi hiyo ilifanyika jana na na iliyoongoza na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Misaada alioyotoa ni pamoja na mchele tani 3.2, Maharage tani 3.4, sabuni za miche za kufulia katoni 50 pamoja na sare za wanafunzi 500, ikiwa ni za wasichana jozi 250 na idadi hiyo hiyo ya jozi kwa wavulana.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Martha Mkupasi, Mbunge wa Chato, Dk. Medard Kalemani, Mkuu wa Gereza la Chato, Raphael Magesa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Batholomew Manunga pamoja na viongozi wa dini, wadau wa maendeleo na wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!