Saturday , 11 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Muhimbili wakana kusambaza video Profesa Jay akiwa ICU
AfyaHabari Mchanganyiko

Muhimbili wakana kusambaza video Profesa Jay akiwa ICU

Spread the love

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imekana kurekodi na kusambaza video ya Msanii wa Bongo fleva, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay anayeendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Video hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inamuonesha Prof Jay ambaye pia Mbunge wa zamani wa Mikumi (Chadema),   akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu (ICU).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 10 Machi, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma – Muhimbili, Aminiel Aligaisha, imesema uongozi wa hospitali umesikitishwa na unalaani kitendo hicho.

“Uongozi wa hospitali, unapenda kuutarifu umma kwamba video hii haijarekodiwa na kusambazwa na hospitali. Tunahudumia wagonjwa takribani 3,400 kwa siku wakiwemo wananchi wa kawaida, viongozi wakuu wa serikali, wanasiasa na watu wengine kwa kuzingatia taaluma, maadili, utu na faragha.

“Tumesikitishwa sana na tunalaani vikali kitendo hiki kilichofanyika cha mtu kurekodi video ya mgonjwa anayepigania uhai wake katika ICU na kuisambaza kinyume na taratibu za hospitali.

“Hiki ni kiwango cha juu cha kukosa utu na maadili. Tunatoa pole kwa mke wa Prof Jay, famiia na jamii nziuma iliyoguswa na tukio hili,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, imewaomba wananchi na watumiaji wa hospitali hiyo kuendelea kuwa na imani pamoja na kuheshimu taratibu za hosptali.

“Tunafuatilia kwa karibu tukio hili ikiwemo kuwasiliana na Mamlaka husika ili kubaini chanzo cha video hiyo ili hatua stahiki zichukuliwe,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waitara ahoji bungeni mwarobaini mauaji katika mgodi Barick North Mara

Spread the loveMBUNGE wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara, ameitaka Serikali kutafuta...

error: Content is protected !!