Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Taasisi kutoa elimu ya sheria, ukatili wa kijinsia
Habari Mchanganyiko

Taasisi kutoa elimu ya sheria, ukatili wa kijinsia

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women and Youth Foundation, Mwanaisha Mndeme
Spread the love

 

TAASISI ya Women and Youth Voice Foundation, imeanzisha program ya kutoa elimu kuhusu sheria na ukatili wa kijinsi kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwanaisha Mndeme wakati akizungumza na gazeti hili, ambapo aliweka bayana kuwa lengo kuu la wao kuanzisha taasisi hii ni kusaidia jamii ya Kitanzania kupata ufahamu wa masuala ya kisheria na ukatili wa kijinsia.

Mndeme amesema kwa siku za karibuni kasi ya jamii kutojua sheria na matukio ya ukatili wa kijinsia yamekuwa yakiongezeka hivyo njia sahihi ya kukabiliana na changamoto hiyo ni kutoa elimu kuanzia ngazi ya shule za awali, msingi na sekondari.

Mkurugenzi huyo amesema katika program hiyo wanatarajia kufikia wanafunzi wa jinsi zote katika shule zaidi ya tano wilayani humo na kwamba mipango yao ni kuwafikia Watanzania wote.

“Tunatarajia kuanzia wiki ijayo, tutaanza kutekeleza program yetu ya kutoa elimu kuhusu masuala ya kisheria na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule takribani tano ambazo ni Kigamboni, Ufukoni, Vijibweni, Kisiwani na Mji Mwema,” amesema.

Amesema imani yao kupitia mafunzo hayo kwa wanafunzi wa shule za msingi, wataweza kubainisha mitazamo kwa kundi hilo ambalo limekuwa likikumbana na changamoto hasa ya ukatili wa kijinsia.

Mkurugenzi huyo amesema katika mafunzo hayo watashirikiana na maofisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri jambo ambalo litaongeza uzito.

Mndeme amesema pia watatumia mafunzo hayo kuwapa wanafunzi motisha na kujiamini ili waweze kutimiza ndoto zao, ambapo wengi wao zinaishia njiani.

“Kuna changamoto kubwa ya makuzi kwa watoto wetu, hivyo naamini kupitia program hii tutaweza kuwafanya wanafunzi kuishi katika ndoto zao,” alisema.

Aidha, mkurugenzi huyo alitoa rai kwa wadau mbalimbali kuwapa ushirikiano ili waweze kufikia malengo yao ya kufikia kila pande ya nchi hasa vijijini ambapo changamoto ya masuala ya sheria na ukatili wa kijinsia vipo.

Mndeme amesema taasisi yao inaamini iwapo kila mdau atashiriki katika utoaji elimu kuhusu sheria na madhara ya ukatili wa kijinsia ni dhahiri kuwa jamii itabadilika na kuishi kwa upendo na amani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!