Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wanawake wajiuza kwa magunia ya mpunga
Habari Mchanganyiko

Wanawake wajiuza kwa magunia ya mpunga

Spread the love

 

TABIA ya baadhi ya wanawake wafanyabiashara ya kujiuza maarufu kama nzige au madanga, kwa malipo ya mpunga, imelalamikiwa na wakazi wa kata ya Nyida, mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania ikitajwa kusababisha migogoro ya kifamilia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).

Hali hiyo ilibainishwa na wakazi wa Nyida mwishoni mwa wiki iliyopita, katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari waliotembelea kata hiyo, kuangalia kiwango cha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Klabu ya waandishi wa habari mkoani hapa, inatekeleza mradi wa nafasi ya vyombo vya habari, kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kupitia ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT).

Wakazi hao walisema kuna tabia ya baadhi ya wanawake wanaotoka mijini kipindi cha mavuno ya mazao, hasa mpunga kwenda kwenye kata hiyo kujiuza kwa wanaume kwa malipo ya magunia ya mpunga.

Wakifafanua, walisema tabia hiyo imekuwa ikiathiri baadhi ya familia kutokana na wanaume wengi kuchukua mazao majumbani na kwenda kuhonga wanawake hao, na kufanya nayo ngono na kusababisha familia kukosa chakula na fedha za kujikimu.

“Kwa kweli sisi kinamama wa Nyinda tunakerwa na tabia ya hawa wanawake wenzetu, wanaotoka miji mbalimbali msimu wa mavuno ya mazao na kufanya biashara “haramu” ya kujiuza.”

“Wanaume wengi kipindi hiki huingia majaribuni kutokana na kushawishiwa na wanawake wasio na aibu hata kidogo, wanafanya ufuska kwa malipo ya magunia ya mpunga, unakuta mwanamume analipa magunia matatu mpaka matano ya mpunga kwa tendo moja, hii ni hatari,” alieleza Esther Bundala.

Slaatiel Joshua alisema wanawake hao, hivi sasa wameanzisha mbinu mpya za kuwaibia wanaume, kwa kumtaka kila anayetaka kuongea kwanza, atoe madebe mawili ya mpunga na wakikubaliana ndipo mwanamume hutoa kati ya magunia mawili hadi matatu ya mpunga ili kufanya tendo la ndoa.

“Hii staili mpya wameipa jina la “Usiniguse” yaani kabla mwanamume hajaongea naye, anatakiwa alipe madebe hayo ya mpunga ndipo waanze kuongea, wakikubaliana, mwanamke huyo anakabidhiwa magunia mawili au matatu ya mpunga, ndipo wanakwenda kufanya tendo la ndoa, tabia hii haifai,” alieleza Slaatiel.

Kutokana na hali hiyo wakazi hao wameiomba Serikali kutunga sheria itakayozuia vitendo hivyo vichafu ambavyo walisema vinachangia kuathiri baadhi ya familia kutokana na kina baba huchukua mazao nyumbani na kwenda kuhonga “Nzige” hao.

Diwani wa Nyida, Selemani Segereti na Ofisa Mtendaji wa kata, Daudi Bonaventura walikiri kuwapo wanawake wanaokwenda kwenye kata hiyo wakati wa mavuno na kufanya biashara ya kujiuza kwa malipo ya mazao, ambao mara nyingi huchukua magunia ya mpunga.

“Ni kweli kwenye kata yetu tuna changamoto hii, lakini tayari tumeanza mikakati ya kuishauri Halmashauri kutunga sheria ndogo itakayobana wanawake wenye tabia hii, na hata hivyo tumeishawaelekeza wenyeviti wa vitongoji na sungusungu kuchukua hatua za kuwafukuza kila wanapowaona,” alieleza Segereti.

2 Comments

  • Si Nyida tu maeneo Kama Ulowa ,Bugomba B Ushetu kina dada hawa hutokea Sana kipindi Cha mavuno Kama Pamba,Tumbaku na hudiriki kujiita eti wajasliamali !

  • Si Nyida tu maeneo Kama Ulowa ,Bugomba B Ushetu kina dada hawa hutokea Sana kipindi Cha mavuno Kama Pamba,Tumbaku na hudiriki kujiita eti wajasliamali !

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!