Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari Wamachinga wampa mapendekezo 5 Rais Samia, awajibu
HabariTangulizi

Wamachinga wampa mapendekezo 5 Rais Samia, awajibu

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo matano, yaliyotolewa na wafanyabiashara wadogo nchini ‘wamachinga’, ili kuiboresha sekta hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kiongozi huyo wa Tanzania ametoa ahadi hiyo leo Jumanne, tarehe 25 Januari 2022, akizungumza na viongozi wa Serikali na wa wamachinga, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mapendekezo hayo ambayo yalitolewa na Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Namoto, ni upatikanaji wa fedha za kukiwezesha chama walichoanzisha cha ushirika wa akiba na mikopo (Machinga Saccos Limited) pamoja na upatikanaji maeneo rafiki ya kufanya biashara.

Mapendekezo mengine ni, kuanzishwa sera na kanuni zinazowatambua rasmi, uwakilishi katika vyombo vya maamuzi na madawati ya wamachinga.

Akizungumzia pendekezo la kutatua changamoto za maeneo ya biashara, Rais Samia amesema Serikali yake imeshaanza kulifanyia kazi, kwa kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha baadhi ya masoko, ikiwemo la Karikakoo.

Amesema ujenzi wake ukikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaidi ya 4,000 ikilinganishwa na idadi ya 2,500 iliyokuwepo awali.

“Nimemwambia Mkuu wa Mkoa (Amos Makalla) tukajenge Jangwani na fedha za kuanzia ujenzi wa Jangwani zipo. Nimwambie Mkuu wa Mkoa aanze kutafuta mkandarasi atakayetujengea Jangwani kwa ramani ambayo mtashirikiana na mtakubaliana,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema, Serikali inaendelea kutafuta maeneo ya wazi, kwa ajili ya kujenga masoko katika maeneo ya pembezoni mwa mji, ili kuondoa msongamano wa wateja katika masoko yaliyokuwepo katikati ya mji.

“Tunahangaika kutafuta fedha, ziwe za ndani, ziwe tutakazopata nje lakini kwa mikopo rahisi, lengo la kufanya hayo masoko tukijua kwamba hata kama tutakopa tutajenga masoko baadae tutakusanya pesa kutoka kwenye masoko, tutarudisha tulikochukua. Tutakopa kwenye mabenki ya ndani ili tufanye hiyo kazi,”amesema Rais Samia.

Kuhusu ombi la fedha za kuiwezesha Saccos ya Machinga, Rais Samia amesema Serikali kupitia fedha za kukabiliana na athari za Ugonjwa wa Virusi vya Korona (Uviko-19), itatoa fedha kwa ajili ya kuiongezea nguvu.

“ Lakini suala la madawati ya sera tutaongea na TAMISEMI, lakini Wizara ya Biashara wakae kitako waone wanakuja na nini katika hilo. Lakini nadhani wizara nzuri ambayo kundi lenu litaingia vizuri, ni Wizara ya Vijana, Kazi na Ajira, kule ndiko tutakaa sera iandikwe kutoka huko,” amesema Rais Samia.

Kuhu uwakilishi katika maeneo mbalimbali Rais Samia amesema watalifikiria.

“Kwa sababu sasa ni kundi maalumu ambalo Serikali inalitambua, lazima muwe na uwakilishi katika maeneo tofauti tofauti,” amesema.

1 Comment

  • Ni vigogo wangapi wa serikali na CCM wamewahi kutembelea mtaa wa Congo na kuona hali ilivyo? Kisha waone mitaa inayozunguka soko la Kariakoo.
    Tuanze na RC Makalla na DC wa Ilala

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari za SiasaTangulizi

Wizara Katiba na Sheria yaliomba Bunge Sh. 441.2 bilioni

Spread the love  WIZARA ya Katiba na Sheria imeliomba Bunge liidhinishe bajeti...

error: Content is protected !!