Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Biashara GGML kuanza kutumia rasmi umeme wa TANESCO mwishoni mwa 2022
Biashara

GGML kuanza kutumia rasmi umeme wa TANESCO mwishoni mwa 2022

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amesema mpango wa kuunganisha umeme wa gridi ya taifa kuelekea katika mgodi wa Geita Gold Mine Limited (GGML) unaendelea ambapo ujenzi wa laini maalumu za kwenda mgodini zimekamilika kwa asilimia 90. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo kubwa cha kupoozea umeme cha Mpomvu kilichopo Mjini Geita ambapo kinauwezo wa Megawatt 90.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo jana mjini Geita kutokana na taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limeshindwa kupeleka umeme unaohitajika na mwekezaji Geita Gold Mine.

Akifafanua zaidi Senyamule alisema kwa upande wa Mgodi (GGML) wanaendelea na hatua za ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha msongo wa Kilovolt 33 kuwa Kilovolt 11 ndani ya mgodi wa GGML chenye uwezo wa Megawatt 40.

“GGML wanatumia voltage level tofauti na inayosambazwa na TANESCO hivyo tunategemea shughuli zote mpaka December 2022 zitakamilika,” alisema.

Mgodi wa GGML unatumia zaidi ya MW 40 zinazozalishwa kwa kutumia jenereta zinazotumia mafuta ya dizeli tangu mwaka 2018.

Hata hivyo, katika mipango ya TANESCO imekuwa ikitekeleza mradi huo wa Mpovu kuhakikisha inapeleke umeme wa zaidi ya MW 20 katika mgodi huo.

Kituo hicho cha Mpomvu chenye eneo lenye ukubwa wa takribani heka tano kitapokea umeme wa Msongo wa Kilovolt 220 na kutoa Kilovolt 33 kisha kuvinufaisha vijiji 11 vitakavyopitiwa na mradi na wakazi 1,424 walio jirani.

Mikoa jirani kama Mwanza na Kagera itaweza kunufaika na umeme huu kwani ni wa kutosha.

Mradi huo mkubwa wa umegharimu zaidi ya Sh bilioni 50 ili kuwezesha wananchi wa Mkoa wa Geita na maeneo ya jirani kupata umeme wa uhakika na gharama nafuu.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa, kukamilika kwa kituo cha kupooza umeme cha Geita kitawezesha Mkoa wa Geita kuwa na umeme wa uhakika utakaowezesha uwekezaji katika sekta mbali mbali hususan  uchimbaji wa Madini na Viwanda.

Kwa upande wake, Kampuni ya GGML imethibitisha kuwa utaratibu wa mananuzi ya mitambo ya kupoozea umeme yaani transformers uko katika hatua ya manunuzi na ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika kufika November 2022.

Makamu Rais wa Kampuni hiyo, Simon Shayo amesema GGML imekamilisha majadiliano na kuandaa rasimu ya mkataba wa kuuziana umeme (power selling agreement) na TANESCO ili kuhakikisha kampuni hiyo inapata umeme wa uhakika na kwa ubora unaotarajiwa ili kuepuka kuathiri shughuli za uzalishaji kwa Kampuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Mchezo wa maokoto Cobra Queen unapatikana Meridianbet

Spread the love Meridianbet Kasino Mtandaoni utapata fursa ya kufurahiamchezo uliochochewa na...

Biashara

Pata Mil 450 ya Non Stop Drop ukicheza Meridianbet kasino

Spread the love  JIUNGE na promosheni ya Kusisimua iitwayo NON-STOP DROP, inayotolewa...

Biashara

Exim Bank yaendeleza malipo ya kidijitali na Chef’s Pride Dodoma

Spread the love  BENKI ya Exim imeingia makubaliano na Mgahawa wa Chef’s...

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

error: Content is protected !!