Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Kesi ya Mbowe: Airtel yabanwa kuhusu ulinzi taarifa za wateja
Habari

Kesi ya Mbowe: Airtel yabanwa kuhusu ulinzi taarifa za wateja

Spread the love

ULINZI juu ya taarifa za wateja umeteka mahojiano kati ya Meneja wa Kitengo cha Sheria cha Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania PLC, Gladys Fimbari na mawakili wa utetezi, katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar ea Salaam…(endelea).

Mahojiano hayo yalifanyika leo Ijumaa, tarehe 14 Januari 2022, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo jijini Dar ea Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Ni baada ya Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala, kumhoji Fimbari kwa nini alitoa taarifa za usajili na miamala ya fedha za namba inayodaiwa kuwa Freema Mbowe, bila kuchukua hatua za kumlinda ikiwemo kwenda mahakamani, kupinga ombi la Kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha Jeshi la Polisi, lililohitaji taarifa hizo kwa ajili ya uchunguzi.

Kibatala alimhoji swali hilo Fimbari, baada ya jana Alhamisi tarehe 13 Januari 2022, akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Esther Martin, kudai barua ya kitengo hicho kwenda kwa Airtel aliipokea tarehe 2 Julai 2020 na kwamba aliijibu na kutekeleza maombi hayo siku hiyo hiyo, kwa niaba ya kampuni hiyo ya mawasiliano.

Kibatala: Nilisikia mnazungumza mambo ya consumer protection or data protection, kipaumbele chenu Airtel ni kumlinda mteja or law complince ikitokea conflict mmoja kuwa custom na law complince

Shahidi: Vyote vinategemea

Kibatala: Kuna Conflict

Shahidi: Always our customer is paramount (kipaumbele) lakini ikiwa issue ya complience mikono yetu inafungwa

Kibatala: Kwa lugha nyingine kama kukiwa na paramount?

Shahidi: Nimesema mteja ni mtu muhimu sana kwetu na tunaangalia sana taarifa zake, lakini pale ambapo tunahitajika kisheria kutoa taarifa za mteja wetu lazima tu-comply ndiyo maana nikasema inategemea

Kibatala: Kama mteja hataki data zake ziwe relaese kwa wasimamizi wa sheria, anataka zitoke, wewe kama mwanasheria wa Airtel unafanyaje. Mtu anasema mimi kiongozi wa upinzani Polisi wanataka kunitengenezea kesi ya ugaidi, kipi boss wako anakipa uzito?

Shahidi: Off course kuna taratibu za kisheria kufuata

Kibatala: On the other hand, unaye mteja wako kiongozi wa chama cha upinzani anasema data zangu uki-release zitakwenda kuwa mis-used , mmepokea order, ipi utaipa umuhimu?

Shahidi: Sifahamu, halafu siwezi kulijibu ni opinion

Kibatala: Unafahamu mteja wako Mbowe ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Chadema? Umetoa taarifa za mtu anaitwa Mbowe, wewe kama wakili unafaham kiongozi wa Chadema hufahamu?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu leo umekuja kutoa ushahidi kwenye kesi gani?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Anashtakiwa kwa kesi gani?

Shahidi: Mpaka nifanye reference

Kibatala: Unafahamu umekuja kutoa ushahidi kwenye kesi gani ama hufahamu?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu ni kesi ya ugaidi?

Shahidi: Hilo silitambui

Kibatala: Kwa uzoefu huo unasema hufahamu kwenye kesi ambayo Mbowe na wenzake wanashtakiwa kwa ugaidi?

Shahidi: Nilishajibu swali

Kibatala: Mwambie Jaji barua imekufikia tarehe ngapi?

Shahidi: Tarehe 2 Julai 2020

Kibatala: Na wewe umeijibu tarehe ngapi?

Shahidi: Tarehe 2 Julai 2020

Kibatala: Sawa sawa na kusema umeijibu siku hiyo hiyo ?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Wakati unapokea barua ile ulifahamu inaomba data za watu miongoni mwa Mbowe ambaye kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Chadema?

Shahidi: Nilivyoisoma hapana

Kibatala: Ulivyoifanyia kazi?

Shahidi: Kwa kuwa niliiona picha

Kibatala: Baada ya kuiona picha ulifahamu hujafaham?

Shahidi: Nilifahamu

Kibatala: Juhudi gani ulizichukua au umeandikiwa barua tarehe tarehe 2 Julai 2020 umeijibu. Juhudi gani umechukua kulinda data za Mbowe?

Shahidi: Imeombwa na chombo cha uchunguzi, taarifa nimeombwa na chombo chunguzi, nilikuwa na jukumu la kutoa

Kibatala: Umeandikiwa barua, imekufikia tarehe 2 Julai 2020, umesema mteja ni mfalme, huu ufalme tunaounaje wa kupoeka barua tarehe hiyo hiyo na unaijibu tarehe hiyohiyo. Nini uliifanya kum-protect?

Shahidi: Chombo kilichoomba taarifa kinaruhusiwa, nilitoa kilichoombwa

Kibatala: Uliipa barua kipaumbele sababu ilitoka kwenye chombo chunguzi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Tukiziangalia barua na matendo yako ni kipengele kipi tutaona Airtel walipofanya wakabalance, tukaona juhudu hii ilikuwa ya kubalance interest ya mteja?

Shahidi: Huwezi kuona

Kibatala: Unafahamu Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA), kifungu cha 6d kinasema nini?

Nyie kama watoa leseni mnatakiwa mbalance haki nyingine za mteja?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Swali langu ni kweli hizo haki zinajumuisha data privacy?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Na hiyo ndiyo sheria uliizungumzia ulipoulizwa na Mtobesya si ndiyo?

Shahidi: Sawa sawa

Kibatala: Kuna sehemu gani mteja haki zake zitupwe kapuni kwa sababu yautekelezaji wa sheria?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu Judiciary Review?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni kesi unaweza ifungua ili ku-challenge amri za umma au nusu umma ukipokea maombi au amri kutoka Polisi ukaweka umuhimu kumlinda mteja wako, unatambua maelekezo hayo kufungua ku-challenge hiyo amri?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kuna kanuni unayoifahamu wewe au sheria mama inaikataza Airtel kwenda mahakamani ku-challenge amri kutoka Polisi ili kumlinda mteja wake?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ni sawa na kusema baada ya kupokea barua kutoka Polisi Airtel walikuwa wanaweza kwenda mahakamani ku-challenge amri, yaani hakuna zuio hilo?

Shahidi: Hakuna zuio hilo

Kibatala: Ulikwenda mahakamani ku-challenge amri ya Polisi ili kumlinda mteja wako?

Shahidi: Sikwenda

Kibatala: Baada ya kupokea barua kutoka Polisi uliwaandikia Polisi kutaka taarifa zaidi kwamba tunatii sheria, tunaomba taarifa kidogo nini kinafanyika?

Shahidi: Hatukufanya hivyo

Kibatala: Mngefanya hivyo mngevunja sheria? Kuna kilichowazuia kufanya hivyo kisheria?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mwambie jaji ni wapi katika barua ya Polisi ambapo mahali iliyosema Airtel tafadhali harakisheni sana mtupe hizi taarifa?

Shahidi: Hamna

Kibatala: Maana yake ni kwamba sio barua wala sio ushahidi wako ambao mahala popote ulionesha kulikuwa na uharaka Airtel kutoa majibu siku hiyohiyo bila kuchukua hatua ya kumlinda mteja wako?

Shahidi: Hakuna

Kufuatia maswali hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando alimtaka atoe ufafanuzi kama ifuatavyo;

Kidando: Ulirejewa kwene zile kanuni chini ya EPOCA na wakakurejea kifu cha 6 (2) kuhusiana na suala la consumer protect, ukasema ni kweli privacy right inatakiwa kuzingatia, ukaendelea kuulizwa haki za mteja zinatupwa kapuni ukasema hapana. Kwa nini ukasema hivyo?

Shahidi: Nilielezea hivyo kwa sababu tunatambua mteja ana haki yake ya usiri wa taarifa zake, lakini ukiweka kifungu cha 6 (2) kinaonesha pale ambapo unaombwa taarifa na mamlaka kutokana na sheria inavyoelekeza, hauna budi kuzito .

Shahidi: Haikuwa jukumu langu kuomba taarifa za ziada kwani vile ambavyo vilikuwa vimeombwa kwa utaratibu wa kisheria na ilinibidi kutekeleza

Kidando: Ulisema barua ya Polisi ilipokelewa tarehe 2 Julai 2021, lakini siku hiyo hiyo ulitoa taarifa hiyo na kwenye barua hailuonesha uharaka wa kutoa hiyo taarifa, kwa nini uliitoa kaa haraka?

Shahidi: Hiyo ndiyo kazi nilipangwa kufanyia kazi, iwe kwa uharaka au kuchelewa. Lakini nilifanyia kazi kwa utaratibu wetu uliokuwa ndani, nilitekeleza kile ambacho kilikuwa kwangu.
B

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!