Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko JK apata pigo, msaidizi wake afariki dunia
Habari Mchanganyiko

JK apata pigo, msaidizi wake afariki dunia

Spread the love

 

OFISI Binafsi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete imethibitisha kutokea kwa kifo cha Katibu wake, Adam Issara kilichotokea jana Jumatatu, Januari 3, 2022 jioni Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarofa iliyotolewa na ofisi hiyo, Issara amefariki akiwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi jijini Dar alipokuwa akipatiwa matibabu ambapo imeelezwa taratibu za msiba na mazishi zitatolewa punde.

“Wakati wa uhai wake, ndugu Adam Issara alikuwa mtu mwaminifu, muadilifu, mchapa kazi hodari na nguzo muhimu ya Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, kabla ya kujiunga na Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu mwaka 2017, Adam Issara alifanya kazi katika iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa Afisa Dawati katika Idara ya Asia na Australia na baadae kuwa Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kati ya mwaka 2007 na 2017.

“Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, na familia yake wanaungana na mjane wa marehemu, Happy Godfrey, familia ya marehemu Adam Issara katika kipindi hiki cha simanzi na maombolezo, Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema, peponi,” Ofisi Binafsi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!