January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Msumbiji, mkewe wakutwa na corona

Spread the love

 

RAIS wa Msumbiji, Filipe Nyusi na mkewe Isaura Nyusi wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona na sasa wamejitenga kwa muda. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya rais nchini humo, Rais Nyusi na mkewe wameamua kujitenga kwa kuzingatia muongozo wa afya baada ya kupatikana na virusi ingawa hawakuonesha dalili zozote.

Taarifa hiyo ilisema waliamua kufanya vipimo baada ya shughuli walizokuwa nazo siku chache zilizopita.

Kumekuwa na ongezeko la virusi vya corona katika siku za hivi karibuni nchini Msumbiji.

Nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu 193,000 wanaougua Covid-19, huku vifo 2,031 vikirekodiwa.

error: Content is protected !!