Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia awalilia 14 waliofariki ajalini, 22 kujeruhiwa
Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 14 waliofariki ajalini, 22 kujeruhiwa

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

WATU 14 wamefariki katika ajali ya barabarani iliyotolea saa 2:15 usiku wa jana Jumapili, tarehe 2 Januari 2022, katika Kijiji cha Lidumbe, wilayani Newala, Mkoa wa Mtwara nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huyo, Mark Njera amesema, chanzo cha ajali hiyo iliyotokea katika barabara ya uchumi, Mtwara-Tandahimba-Newala-Masasi ni mwendokasi wa dereva wa gari aina ya Scania wakati aliposhindwa kulimudu na kwenda kuwagonga watu hao hali iliyosababisha vifo na majeruhi ya watu 22.

Kufuatia vifo hivyo, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametua salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Gugati akimtaka kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa na marafdiki na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Rais Samia pia amewaombea kwa Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wote mahali peni peponi amani.

Aidha, Rais Samia amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama barabarani, kuongeza juhudi za kudhibiti ajali hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka na pia amewaasa madereva kufuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!