Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Biashara Benki ya Exim yaendelea kutangaza washindi wa droo ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’
Biashara

Benki ya Exim yaendelea kutangaza washindi wa droo ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’

Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim, Agnes Kaganda, (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa zoezi la uendeshaji wa droo ya kuwatafuta washindi wa droo ya pili ya kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’. Wengine ni ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Neema Tatock (Kulia) na Meneja Msaidizi wa Bidhaa za Rejareja kutoka benki hiyo, Callist Butinga (Kushoto)
Spread the love

Benki ya Exim imetangaza washindi wa droo ya pili  ya  kampeni  ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe! ’inayoendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana huku wakipata fursa za kunyakua zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu pamoja na gari aina Toyota Vanguard. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Akitangaza washindi wa droo hiyo  iliyofanyika leo tarehe 3 Januari, 2022jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim, Agnes Kaganda, alisema jumla ya washindi 6 walipatikana kupitia droo hiyo na kujishindia zawadi ya shillingi million sita fedha taslimu.

“Katika droo ya leo jumla ya washindi sita (6) wamepatikana  ambao ni Manish Govindji, Abdulkarim Lema, Emashu Investment, Paul Kadonya, Emile Singano, Ibrahim Nyange na Pritipal Chadha na hivyo wameweza kujishindia zawadi za fedha taslimu kiasi cha sh mil 6. ” alitaja

Washindi hawa sita kwa mujibu wa Kaganda watakabidhiwa zawadi zao katika maeneo yao waliopo huku akibainisha kuwa benki hiyo itaendelea na droo kama hizi kila mwezi na washindi wataendelea kuingia kwenye droo itakayowawezesha kushinda zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota Vanguard.

“Wateja wetu wa sasa na wale wapya watakuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi hizi kila watakapojiwekea akiba ya kuanzia Tsh. 500,000 na kuendelea. Kadili wanavyojiwekea amana kubwa zaidi ndivyo wanavyojiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi kubwa zaidi,’’ alisema Kaganda wakati wa droo hiyo iliyohudhuriwa pia na muwakilishi kutoka  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini.

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo Kaganda alisema inalenga kuleta mabadiliko kwenye mtazamo wa uhifadhi wa amana miongoni mwa watanzania kutoka kuhifadhi pesa majumbani na badala yake wazihifadhi kupitia benki hiyo kwa usalama wa fedha zao sambamba na faida nyingine nyingi ikiwemo riba.

“Lengo si tu kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea amana, tunachohitaji ni kuona kwamba Watanzania wengi wanajiwekea amana zao sehemu salama ili kujiendeleza kukua kiuchumi ndio maana tumejipanga kuwahamasisha watumie akaunti zetu mbalimbali ikiwemo akaunti ya mshahara inayotumika kwa matumizi mbalimbali ya kila siku,’’ alitaja.

Alitaja akaunti nyingine kuwa ni pamoja na akaunti ya mzalendo inayoendeshwa bila makato ya kila mwezi, akaunti ya haba na haba, akaunti ya faida ambayo inakuruhusu kuweka akiba na kupata riba pamoja na akaunti ya Nyota ambayo ni akaunti maalum kwa ajili ya Watoto pamoja na akaunti ya wajasiriamali inayowahudumia wafanyabiashara na mahitaji yao tofauti tofauti ya kibiashara.

Kwa upande wake  Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Neema Tatock alitoa pongezi kwa washindi wa promosheni hiyo huku akiwahamasisha walengwa kushiriki kwa wingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata huku akiwahakikishia kuwa Bodi hiyo imejipanga kuhakikisha zoezi la kupata washindi linafanyika kwa kwa uwazi na kwa kufuata misingi halali ya kubahatisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Shinda mpaka 1,250,000/= ukicheza shindano la Expanse Kasino

Spread the love  KUBWA zaidi kutoka Meridianbet ni promosheni ya Expanse ambayo...

Biashara

Miaka 20 iliyopita luninga ilikuwa ni ishara ya utajiri

Spread the love  UKINIULIZA nikutajie idadi ya vifaa vya umeme mashuhuri vilivyokuwa...

Biashara

Malipo kwa njia 40 ndani ya sloti ya Lucky Sevens kasino 

Spread the love  IRINGA na Tanga Lushoto husifika kwa uzalishaji wa mtaunda...

Biashara

Njia 100 za ushindi na Fruit Salad 100 kasino 

Spread the love  Ni wakati mwingine tena wa kufahamu kuhusu Michezo ya...

error: Content is protected !!